Huo ndio uchafu uliotupwa katika kijiji cha shenda siku ya tarehe 9 Disemba ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima
|
Krantz Mwantepele,Geita
Wananchi
wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani
Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa
takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9
Lililofanyika nchi nzima.
Wakiongea
na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao
wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutupa
takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo
hilo.
Wameongeza
kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la
shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua
hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza
na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.
Sambamba
na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri
kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya
wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa
kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.
Kwa
mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema
sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza
kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu
hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.
Kwa
upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe…………..amesema
kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu
katika taka hizo na kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa
na madhara kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment