Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Tarime Vijijini uliofanyika Novemba 25,2015. Kesi hiyo ilifunguliwa aliekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye akiiomba Mahakama kutengua Ushindi wa Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche aliechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa January 19,2015 chini ya Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha leo imeahirishwa hadi kesho January 28,2015 majira ya saa nane mchana itakapotolewa maamuzi yake.
Mjibu maombi katika kesi hiyo (John Heche) anawakilishwa na Mawakili Tundu Lisu (leo hakuwa Mahakamani) pamoja na Paul Kipeja (alikuwepo Mahakamani).
Baada ya Kesi hiyo Kuahirishwa, Katibu wa Chadema Mkoani Mara Mwl.Chacha Heche (Pichani Juu anaehojiwa) ameiomba Mahakama kutoa maamuzi ya Kesi hiyo ili kuwapunguzia gharama kwa kuwa ambazo zinajitokeza wakiwa Jijini Mwanza kufuatilia maamuzi ya kesi hiyo.
Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa amesema kuwa wanatarime vijijini wana imani na Mahakama na kwamba kesi hiyo ni sehemu ya changamoto kwa mbunge wao na kwamba wembe ni ule ule wa kushinda kuanzia jimboni hadi Mahakamani.
Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa.
Paul Kipeja ambae ni Wakili upande wa Mjibu Maoni akizungumza na wanahabari baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuahirisha kutoa Maamuzi ya kesi ya Kupinga Matokeo Jimbo la Tarime Vijijini.
Anasema kama ilivyokuwa katika Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na Wapiga kura wa Jimbo hilo dhidi ya Esther Bulaya (Mbunge), ndivyo itakavyokuwa hata katika Jimbo la Tarime Vijijini kwa maana ya mteja wao (John Heche) kushinda kesi inayomkabiri.
Tazama HAPAPicha katika Siku ya Kusikiliza Kesi Hiyo.
0 comments:
Post a Comment