https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    List ya majina ya wachezaji wanne wanaoweza kutwaa Ballon d’Or ukiondoa Messi na Ronaldo …

    January 20 imenifikia list ya majina manne ya wachezaji wanaopewa nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or, baada ya Messi na Ronaldo. Ikiwa ni siku 9 zimepita toka shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limtangaze mchezaji wa kimataifa waArgentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano. Hii ndio list ya majina ya wachezaji wanaotajwa kupewa nafasi ya kutwaa Ballon d’Or baada ya Messi na Ronaldo.
    4- Anthony Martial wa Man United licha ya kuwa na umri wa miaka 19, uwezo na umahiri wake wa kucheka na nyavu unaaminika kuwa utakuwa na kumfanya awe mchezaji bora wa dunia, kwani uwezo wake anaouonesha sahizi unafanya wengi kutarajiwa makubwa kutoka kwake.
    Manchester United's Anthony Martial scores past Liverpool's Simon Mignolet during the English Premier League soccer match between Manchester United and Liverpool at Old Trafford Stadium, Manchester, England, Saturday, Sept. 12, 2015. (AP Photo/Jon Super)
    3- Eden Hazard wa Chelsea ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu kwa msimu uliyopita, alionekana kuwa na uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi kuliko kufunga, hilo linatajwa kuwa suala la mpito ila uwezo wake mkubwa unfanya watu wamtabirie makubwa.
    Hazard13
    2- Luis Suarez
    Baada ya majina matatu ya mwisho ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2015 kutajwa, wakiwa NeymarMessi na Ronaldo, staa wa soka wa BrazilNeymar ndio alikuwa wa kwanza kutoka hadharani na kusema kuwa Luis Suarezalistahili kuwepo miongoni mwa majina matatu.
    Suarez9
    1- Neymar
    Ni ukweli usiofichika kuwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanabidi wajipange kwa staa wa soka wa Brazil na nahodha wa timu hiyo Neymar, kwani anaonekana kuja juu kwa kasi. Neymar katika umri wake wa miaka 23, amefanikiwa kufunga magoli 209 katika michezo 341 kwa vilabu vyote alivyowahi kuchezea. Hii ni dalili ya nyota huyo kuja kufanya vizur kwa siku za karibuni.
    Neymar14

    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: List ya majina ya wachezaji wanne wanaoweza kutwaa Ballon d’Or ukiondoa Messi na Ronaldo … Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top