https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO


    Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif Picha na SUPER D BOXING NEWS
    Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Sharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
    KIONGOZI KUTOKA KATIKA KAMPUNI YA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU
    Promota wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
    BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI KUTOKA NGUMI ZA KULIPWA PST PEMBE NDAVA

    Na Mwandishi Wetu
    MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59
    Akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini

    unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni

    na Baina Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa

    nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini

    nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu

    Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

    pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top