Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Uganda, Injinia Badru Kiggundu asubuhi ya leo ametoa taarifa za matokeo ya uchaguzi wa rais katika vituo 6,448 ambapo yanaonyesha rais Yoweri Museveni anaongoza.
Matokeo yanaonyesha rais Yoweri Museveni wa NRM anaongoza kwa kura 1,362,961 sawa na asilimia 61.75 na mpinzani wake wa chama cha FDC Kizza Besigye kapata kura 738,628 sawa na asilimia 33.47.
Jumla ya wapiga kura 15,277,198 walitarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo mkuu wenye ushindani mkali nchini Uganda, ambao ulikuwa na vituo 28,010 vya kupigia kura.
Mgombea urais Dk. Kizza Besigye akitafakari mbele ya sanduku la kupigia kura
Rais Yoweri Museveni mwenye kofia ya pama pamoja na mkewe Janet nyuma yake wakiwa katika foleni ya kupiga kura jana.
0 comments:
Post a Comment