Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Tigo wa duka jipya la Tigo Tunduma mara ,baada ya hafla ya ufunguzi wa duka jipya la Tigo katika mji wa Tunduma Mkoani Mbeya mapema wiki iliyopita
Kampuni ya simu ya Tigo imefungua duka jipya Tunduma ambalo limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kusini Bw.Jackson Kiswaga alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.
"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Tunduma ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu za mkononi"Alisema Kiswaga.
Kiswaga alisema kuwa duka hilo linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.
Kwa upande wa katibu wa mkuu wa wilaya ya Tunduma Mhe. Richard Mbeho alipongeza hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya Tunduma.
|
0 comments:
Post a Comment