Baraza maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara limewasimamisha kazi watumishi wanne wa Halmashauri hiyo akiwemo Mweka hazina wa Halmashauri hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Halmashauri ya wilaya hiyo.
Aidha, katika maamuzi yake Baraza hilo limesema halina imani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Bwana Felix Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wa zaidi ya shilingi milioni 83 na hivyo kupendekeza kwenye mamlaka zinazohusika kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazomkabili.
Hata hivyo mkutano huo maalumu nusura uingie dosari baada ya mkuu wa wilaya ya Hanang, Bwana Thobias Mwilapwa kuingia ukumbini na kutaka kumtetea Mkurugenzi mtendaji huyo,huku akiwatishia wajumbe wa mkutano huo kwamba mkutano haukuwa halali na ndipo mambo yalikuwa hivi.
Kikao hicho kilichotakiwa kuanza majira ya saa nne asubuhi kililazimika kuanza majira ya saa sita mchana kutoka na wajumbe wa mkutano huo kumsubiri katibu wa kisheria wa mkutano huo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kwa saa mbili bila mafanikio,zaidi ya kumtumia Mkuu wa wilaya,Bwana Thobiasi Mwilapwa ambaye hata hivyo alijikuta akitolewa nje ya ukumbi huo.
0 comments:
Post a Comment