https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    RAIS BARACK OBAMA NA MKEWE MICHELLE WASAKATA MUZIKI WA TANGO ARGENTINA


    Rais Barack Obama na Mkewe Michelle wamekuwa na wakati mzuri nchini Argentina ambapo wameonekana wakisakata muziki wa aina ya Tango Jijini Buenos Aires wakati wa hafla ya mlo wa usiku walioandaliwa na mwenyeji wao.

    Rais Obama yupo Buenos Aires kukutana na kiongozi wa Argentina Mauricio Marcri baada ya kumaliza ziara yake ya Cuba, na amekuwa akipuuzia wito wa kumtaka kurejea Marekani kufuatia mashambulizi ya Jijini Brussels, Ubelgiji.

    Rais Obama ambaye amesema hakubali magaidi waharibu ratiba yake alionekana jana usiku akicheza katika mlo alioandaliwa na Ikulu ya Argentina akiwa na mkewe Michelle pamoja na mke wa rais wa Argentina Juliana Awada.
                                             Rais Obama akionyesha kuimudu miondoko ya Tango
                     Naam mambo ya Tango hayo rais Obama akienda nayo sambamba 


    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RAIS BARACK OBAMA NA MKEWE MICHELLE WASAKATA MUZIKI WA TANGO ARGENTINA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top