Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionyeshwa
eneo la uwanja wa ndege itakakopita barabara ya Mchepuko itakayotoka
Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi
Duga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua eneo
ambalo barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda
Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo
kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa
barabara ya mchepuko.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo
kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa
barabara ya mchepuko.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua
jambo katika makutano ya barabara ya mchepuko eneo la Duga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama
ramani ya gati ya Bandari ya pangani ambayo inajengwa kwa gharama ya sh.
bilioni 2.3.
Muonekano wa gati inayojengwa katika bandari ya Pangani iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.3.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama
ramani ya daraja la Mto Pangani ambalo upembuzi yakinifu wa ujenzi wake
umekamilika na litaanza kujengwa hivi karibuni.
…………………………………………………
SERIKALI
ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya
Tanga,Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa
kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tayari kazi iliyobaki ni kupata
mzabuni wa kuendesha mradi huo.
Waziri
wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa
ujenzi wa Barabara hiyo utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka
wa fedha 2016/2017 na kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na Benki ya
Maendeleo ya Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.
Mradi
huo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja katika Mto Pangani lenye urefu
wa mita 550 ambalo linategemewa kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya
kuimarisha shughuli za utalii katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Kwa
mujibu wa Prof.Mbarawa ni kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo
serikali itawalipa fidia wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa
tathimini kwa mujibu wa sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2009.
“Nasisitiza
kwamba kama sheria inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai
kila mwenye haki na anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili
hatalipwa na hii itakuwa ni kulingana na tathmini
iliyokwishafanyika……”,alisema Waziri huyo.
Alisema
kuwa serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa Barabara hiyo kwamba ndiyo
kiini na moyo wa uchumi wa wilaya ya Pangani hasa kwa kutambua namna
ambavyo ina vivutio vingi vya kitalii hatua itakayolenga kuwaongezea
fursa za kibiashara wananchi na kukuza Pato lao.
“Daraja
hili litakuwa na uwezo wa kupitisha magari na watembea kwa miguu kwa
wakati mmoja na hivyo ni mkombozi wa wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa
walikuwa wakitegemea kuvuka ng’ambo ya pili ya mto kwa kutumia kivuko tu
ambacho wakati mwingine kinakumbwa na hitilafu”,alifafanua Prof.Mbarawa
ambaye yupo mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.
Akizungumza
wakati wa majumuisho ya ziara yake baada ya kukagua Kivuko cha Mto
Pangani,Barabara ya Tanga,Saadani mpaka Bagamoyo na eneo linalotakiwa
kujengwa Daraja,Prof.Mbarawa aliuagiza Uongozi wa Wakala wa ufundi na
Umeme(Temesa)kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za utendaji wa kivuko kwa
kila siku.
Aliwaagiza
kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya elektroniki ili kuepusha vitendo
vya ubadhirifu wa fedha wakati serikali ikiwa kwenye mpango wa
ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Suala
la kutumia mashine za kieletroniki halina mjadala habari ya kutumia
vitabu vya risiti ili muongeze sifuri mbele hatuzitaki….hapa kuna shida
kuna siku I naandikwa imeingia shilingi milioni moja lakini Benki
zimeenda laki nane na hamsini hii laki moja na hamsini zinaishia wapi
hili ni tatizo”,alisema.
Hata
hivyo alisema ipo haja kwa Temesa kuajiri manahodha wa vivuko ambao
wanafanya kazi kwa viwango vya kitaaluma ambavyo vinakubalika badala ya
kutumia Wazee ambao wanafanya kazi kwa mazoea.
0 comments:
Post a Comment