https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    BARCA YA LOUIS ENRIQUE NA MAISHA BAADA YA XAVI HERNANDEZ

    Xavi-Enrique
    Xavi-Enrique
    Kwenye moja ya makala zangu hapa, makala iliyokua inamuelezea  Thaban Kamusoko niliahidi ipo siku nitagusia namna Spain na Barca walivyolazimika kubadili style ya uchezaji wao kwa kiasi fulani ili kuziba pengo la Xavi Hernandez ‘midfield general’, master wa tik-taka kiungo ambaye kwa uwezo wake wa pasi zake, ‘intelligent’, maono aliyokua nayo uwanjani alikua na uwezo wa ku-boss midfield yeyote duniani enzi za ubora wake.
    Hakuna timu ilishawahi kutana na Xavi katika ubora wake wakatoka salama, unabisha? kaulize alivyokifanya kiungo cha Real Madrid kilichokua na wakali kama Xabi Alonso, Sammy Khedira, na Mesut Ozil pale Nou Camp wakati wanakula 5 au kaulize alichowafanya Ujerumani ya wakali kama Bastian, Khedila na Ozil Euro 2008 na World Cup 2010 pale South Africa au usipoteze muda kuvuta sana kumbukumbu kumbuka tu alichowafanya Italy ya kina Pirlo, Claude Marchisio na Ricardo Montolivo Euro 2014 wakati wanapigwa 4.
    Xavi ni aina ya viugngo waliokua wamejaaliwa karibu kila kitu enzi za uchezaji wao japo mwenyewe anaamini kiungo aliyekua amekamilika zaidi ni Paul Scholes, kwake Scholes ni complete package huwezi pinga maoni yake hayo kuhusu Scholes kwani ni maoni anayo share na mashabiki, wachambuzi, makocha na magwiji mbalimbali wa soka ambao kwa nyakati fofauti wamewahi mmwagia sifa Scholes.
    Ukijaribu kuwafananisha magwiji hao wawili kuna mengi ya kufanana, pass selections, composure, close control, vision, japo Scholes aliongezea tenacity (uwezo wa kunyang’anya mipira), box to box na uwezo wa kunusa goli kuliko Xavi na kumfanya Scholese kukamilika zaidi na hivyo kuwa na uwezo wa kufanya chochote katikati ya uwanja ila ukiacha ukweli huo huwezi kukataa ukweli mwingne kwamba Xavi kuna baadhi ya maeneo alikua bora kuliko hata Scholes.
    Uzuri wa Xavi alikuwa najua vitu vichache lakini alikuwa anavijua sana na alivifanya kwa ubora mkubwa sana ni kama Professor anaejua kitu kimoja kama ni History basi anaijua hasa ukimtoa nje ya History hakuna anachojua wenzetu wanaita ‘pipeline knowledge’.
    Mfano Xavi alikua anajua sana ku-control tempo ya timu yake na timu pinzani kuliko kiungo yeyote nimewahi mshuhudia kwa macho yangu, sina maana kina Scholes na wengne hawajui ninachomaanisha Xavi aliweza zaidi eneo hili kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kuchagua machaguo ya upigaji pass uwanjani (pass selection), vision na timing yake, tactical awareness (uwezo wa kusoma mchezo) anapokua na mpira, pasi gani, ipigwe wapi, muda na kwa sababu gani (what pass, where, when and why)
    Uwezo wake huo uliwafanya wanaomzunguka kuwa huru zaidi kwani angeweza kutengeneza nafasi hata kwenye midfield iliyo compact kiasi gani, kwa mfano Xavi angeweza kupokea mpira akakaanao mguuni sekunde kadhaa akisubiri wachezaji kadhaa  wa timu pinzani waje kuweka pressure kwenye mpira wakiamini wanaweza mnyang’anya lakini Xavi kwa timing ya kipekee aliyokuanayo angeweza uachia mpira  kuelekea kwa mchezaji mwenzake mara nyingi anakua Iniesta bila shaka tunakumbuka zile “Xavi to Iniesta, Iniesta to Xavi, Xavi again”.
    Kabla ya wachezaji husika hawajafika kwenye mpira, kwa kufanya hivyo wachezaji wawili ama watatu watakuwa wameacha maeneo yao wamejikuta wamekusanyika kwa mtu mmoja lakini mbaya zaidi wamepishana na mpira na hivyo maeneo yao waliyoyaacha sasa yangeweza tumika vema na wachezaji wajanja kama Messi,Iniesta, Pedro na D.Villa kuwadhuru, huo ni urahisi unaoupata ukicheza na Xavi.
    Kingne ni uwezo wa kuamua muda gani timu yake iende kwa kasi golini kwa mpinzani kutafuta goli, muda gani wamiliki tu mpira kama njia ya kujilinda kwa kupunguza presure ya mpinzani. Ni kwa ubora wake huo kocha wake wa timu ya taifa(Spain) amewahi sikika akisema siku ya kumuaga (Xavi testimonial) kwamba, kuna wakati “Xavi alikua vital cog kwenye tik-taka ya Spain kuliko hata kocha” maneno mazito lakini ni wazi  ni ya kweli na yalilenga kuonesha umuhimu wa Xavi kwenye ubora wake.
    Inapotokea unampoteza mchezaji wa ubora na umuhimu wa Xavi kwenye kikosi chako, umbwe (void) analoliacha huchukua muda kuzibwa kama hatua stahiki hazitachuliwa, tuna mifano kadhaa ya timu kwa zilivyowahi pata shida kuziba mashimo yaliyoachwa na wachezaji mihmu, Gerard pale Lliverpool, Keane na Scholes pale United na Viera wa Arsenal.
    Kwa kawaida unapofikiria mabadiliko unafikiria vitu viwili, unafikiria mabadiliko makubwa au madogo, wenzetu husema ”when you think of changes you think of either evolution or revolution”, evolution kwa maana ya kubadili sehemu ndogo tu ya system/team mfano, unaweza nunua mchezaji mpya mwenye sifa za kama aliyeondoka au revolution kubadili mfumo mzima wa uchezaji baada ya kukosa mchezaji mwenye sifa za kama aliyeondoka, Spain na Barca walilazimika kufanya hii chaguo la pili la revolution kwani kwa Barca mfano licha ya uwezo wao si Rakitic wala Arda Turan anaweza kuwa Xavi.
    Ndiyo maana ukiiangalia Barca ya Louis Enrique kwa makini utagundua kuna tofauti ya kimsingi na ile ya Pep Guardiola, kuna sababu kadhaa kwa nini? lakini kubwa zaidi ni kwamba Xavi yuko anaota jua na kula tende Uarabuni badala ya kuwa kwenye glisi ndani ya chumba cha injini ya Barca
    Pep aliijenga Barca ya La Masia haswa, kila kitu walichokifanya kilikua kwenye triangles, kuanzia kupasiana pasi fupifupi wakati wa kushambulia ama kuzuia, ku-press, kufungua defense ya timu pinzani n.k alihakikisha kuna wachezaji watatu wanaoshirikiana kila eneo, tulizoea kuiona triangle ya Danny Alves, Messi na Xavi , upande mwingne Iniesta, Messi, D.Villa au Pedro katikati Xavi, Iniesta na Bousquet wakati wa bulid up play nyuma kabisa unamkuta Pique, Valdes na Puyol.
    Kwenye hizo triangle zote ni wazi kuna jina moja litatokea sana Messi na hiyo ni kutokana na role aliyokua anaicheza uwanjani alikua ana float free akiwa huru kwenda kokote uwanjani, kulia katikati na kushoto kwa kifupi kwenye maeneo yote  ya mbele  mahala palipo kua panakosekana mtu wa tatu messi alipaswa kua mtu huyo wa tatu, wenzetu wanasema ni mchezaji aliyekua “anapick up the missing pieces uwanjani”  tringle hizo hazionekani sana Barca ya sasa.
    Lakini tofauti nyingne kubwa iliyopo Barca ya sasa na ile ya Pep, Barca ya Pep ilikua ina press kwa haraka kwenye triangles kila wanaponyang’anywa mpira, kwenye kila tringle tajwa hapo juu kulikua na mtu wa kwanza kuweka pressure kwenye mpira akisaidiwa na wenzie, huyu mtu anaitwa (peers of pressing) Alves, Pedro na Puyol ni mifano ya peer of pressing kwenye trangles zao, ndiyo maana enzi za pep tofauti na Barca ya sasa ilikua aghalabu timu pinzani kukaa na mpira kwani kila waliponyang’anywa walipress kwenye triangle kama siafu.
    Barca ninayoiona ya Enrique hawako obsessed na  kumiliki mpira kwa pass fupifupi kwa  kushambulia ama ku press kwenye triangles, wenyewe wanacheza expansive football/continental football mpira wa kucheza kwa nafasi, pasi ndefundefu na kucheza kutumia uwezo binafsi zaidi kuliko system kupata matokeo ndiyo maana kwa kiasi kikubwa hatuzioni triangle za Pep. Hii ni style iliyowahi tumika miaka ya nyuma timu zilizowahi kuwa bora sana ni Madrid ya mwanzoni mwa 2000’s na Brazil pia mara kadhaa huko nyuma.
    Expansive football ya sasa ya Barca ina faida na hasara zake, faida kwa mfano ni kwamba kwa style hii timu inaposhambulia hufikia haraka goli la mpinzani kwani hushambulia kwa pasi ndefu kwani sasa sehemu ya kupiga pasi mbili au tatu inapigwa pasi moja na kuondokana na kitu wanaita “one pass way too many” faida nyingne ni kwamba hii ni style inayowapa uhuru wachezaji wenye vipaji vyao kuonesha uwezo wao, style hii inawafaa zaidi wachezaji waliopo Barca sasa kwani haiwalazimu kumiliki mpira kwa muda mrefu, unawezaje kulazimisha kumiliki mpira ukiwa hauna Xavi katikati ya uwanja?
    Rakitic ni mchezaji mzuri lakini hata kwa maneno yake mwenyewe amewahi kukiri kuwa kazi yake kubwa ni ku-cover ground uwanjani si kusaidia timu kumiliki mpira kwani anajua licha ya kununuliwa kucheza mahala pa Xavi lakini hata kuja kuwa Xavi, Rakitic kwa mfano tofauti na Xavi aliyekua kama ‘amphibia’ akiwa na uwezo wa kuishi kote majini na nchi kavu Rakitic anaweza cheza zaidi kwenye high tempo (pale timu inapocheza kwa kasi) zaidi kuliko wanapocheza taratibu.
    Ndiyo maana sioni ajabu timu kucheza na Barca ya sasa ikamiliki mpira kuliko Barca na kutengeneza nafasi za kutosha dhidi yao sababu Barca hii hawana Xavi lakini pia hawamiliki mpira wala ku-press kwenye triangles, kwa kifupi unaweza sema Barca ya sasa imechanganya tik-taka na counter attack na kupata expansive football mfumo unaofurahisha kuutazama lakini si salama sana kwani huwapa pia timu pinzani fursa ya kushambulia na kutengeneza nafasi.
    Kipindi kama hiki ambacho Barca wanaonekana kuishiwa nishati na kuandamwa na fatique kutokana na wingi wa mechi walimuhitaji zaidi Xavi kuwasaidia kutumia vema nishati ndogo iliyobaki kuwavusha kipindi hiki muhmu kwenye msimu wao, Xavi angeweza kuchagua muda gani wacheze taratibu kulinda nishati na wakati gani muafaka waitumie kupata matokeo.
    Kwenye mchezo wao wa marudiono wa Champions League dhidi ya Atletico, Atletico wakitengeneza nafasi kama nilivyoonesha hapo juu na walifanikiwa ku-excute plan plan yao. Umakini, juhudi zao na namna walivyoweka pressure kwenye mpira (intesity) wakafanikiwa kushinda game, wakati kwa Barca ya sasa inategemea namna MSN wakavyoamka na kiasi gani wameliifadhi nishati kuelekea mchezo huo ni wazi mechi haukuishia Nou Camp.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA YA LOUIS ENRIQUE NA MAISHA BAADA YA XAVI HERNANDEZ Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top