1. MSN 0-1 BBC, Ni dhahiri na wazi kabisa huu haukuwa usiku wa Messi-Suarez-Neymar, utatu huu leo ulikuwa kimya ukiachana na mashambulizi ya hapa na pale, BBC kwa ujumla wao ndiyo waliopeleka kilio Catalunya.
2. Rakitic-Busquets-Iniesta, ukiachana na wale watatu wa mbele, hawa ndiyo injini ya Barcelona kwasasa, hawa ndiyo wanaoamua namna ya timu kucheza na namna ya timu kuzuia. Hawa ndiyo wabeba maji kwaajili ya MSN.
3. Magoli ya MSN yanafanya makosa ya Pique, Mascherano, Alba na Alves kutembea kwenye kivuli hicho, ukuta wa Barcelona sio bora na kama Madrid wangekuwa makini zaidi usiku wa leo basi magoli mengi zaidi yangepatikana.
4. Jina lake ni EL CLASICO, mchezo uliotarajiwa kutazamwa na nchi 184, mashabiki kwa ujumla waliotarajiwa kutazama ni milioni 600 lakini haikuwa SHOW nzuri sana kustahili watu wote hao hasa kipindi cha kwanza. Kuna mahali ilikuwa ni kama mchezo wa kugombania kombe la mfalme.
5. Asante na kwaheri Johan Cruyff, dakika ya 14 ya mchezo wa leo mashabiki walisimama na kwa umoja wao wakapiga makofi bila kujali ni mashabiki wa klabu gani. Asante kwa kutuletea soka hili la "nipe nikupe halafu nipe tena na nikupe tena".
6. Mchezaji aliyemfukuzisha kazi Benitez ndiye aliyempa Zidane sifa leo, CASEMIRO kwenye mchezo wa kwanza wa el clasico Benitez alimweka nje na matokeo yake tunayajua, huyu ndiye leo alikuwa silaha ya Zidane dhidi ya MSN, mshikaji alikubali kuwa "mbeba maji" na mkata umeme tu.
7. Luka Modric, kwangu huyu ndiye "MOTM", mshikaji aliupiga mpira mwingi sana, vita ya katikati ya uwanja huyu ndiye aliyeibuka mbabe leo, kuanzia kuiondoa Madrid nyuma na kuongeza mashambulizi eneo la mbele.
8. ZIDANE 1-0 PEREZ, matokeo ya el clasico ndiyo ambayo huamua maisha marefu ama mafupi ndani ya Madrid, na leo Zidane ameibuka kidedea dhidi ya mwamuzi wa maisha yake ya baadaye ndani ya Madrid. Mbinu ya kuisubiria Barcelona na kuishambulia kwa mipira ya kushtukiza (counter attack) imemlipa Zizou.
9. Marcelo Vieira, hivi kuna beki wa kushoto anayeshambulia kama huyu jamaa duniani? kitu kikubwa ambacho amepewa na mabeki wengi kunyima ni umahiri wa miguu yake (foot work) akitaka kukupiga chenga atakupiga na akitaka kukokota mpira ataukokota bila kusita, goli la kwanza la Madrid lilitokana na shughuli yake.
10. Cristiano vs Ramos, The beauty vs The beast. Hawa ni wachezaji wawili wa Real Madrid ambao mchanganyiko wao leo ndiyo uliopeleka ushindi Madrid, wakati upande mmoja ukifunga goli la ushindi upande mwingine ulifanya kazi ya kuzuia magoli zaidi na mpaka kupewa kadi nyekundu lakini nani anajali. Magoli 29 ya Ronaldo ndani ya la liga sio jambo dogo hasa wapinzani wakiwa ni MSN na zaidi ukikumbuka ile penati ya Kicruyff.
0 comments:
Post a Comment