https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza



    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    Dar es Salaam, 12 Aprili 2016-Shirika la ndege la bei nafuu, fastjet, limetangaza punguzo la nauli la sh. 22,000/- kwa mwezi huu wa Aprili kwenye safari zake za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza.

    Kulingana na Afisa Masoko na Uhusiano wa Umma wa fastjet, Lucy Mbogoro, ofa hiyo ijulikanayo kama JET10 imeanza kuanzia mwanzo wa April na itamalizika tarehe 30 Aprili 2016.

    “Ofa hii kutoka fastjet inaashiria kwa mara nyingine tena jinsi shirika letu linavyosikiliza matakwa ya wateja wake”, alisema Mbogoro.

    Mbogoro alisema kwamba wateja wanaweza kilipia nauli zao kupitia mitandao ya Tigo-Pesa, Airtel Money, M-Pesa and pia kupitia NMB Mobile Cash katika tawi lolote la Benki ya NMB.

    “Wateja wanashauriwa kukata tiketi mapema ili kufurahia nauli za bei nafuu zaidi na pia wanaweza kulipia kupitia m.fastjet.com or www.fastjet.com.” alishauri Mbogoro.


    Mwisho 



    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top