WANAMUZIKI Kadijanito au ukipenda muite Kadja amefunguka kuwa, anawashangaa sana wanaomfananisha uwezo wake wa kuimba na alio nao mwenzake kutoka THT, Rubby.
Kadja aliiambia safu hii kuwa, anajua uwezo wake wa kimuziki uko juu, hivyo wanaomlinganisha na Rubby wamekosa kazi ya kufanya.
“Unajua mimi najijua niko levo gani, sijisifii ila mimi siyo levo za akina Ruby, yule ni cha mtoto kabisa kwangu hivyo najisikia vibaya sana pale mtu anapofikia hatua ya kunifananisha naye.
Kadja sasa anafanya poa na wimbo wake wa Sina Maringo ambao ameshaufanyia kichupa.
0 comments:
Post a Comment