Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi, Memphis Depay atakua na hasara ya kukosa kiasi cha paun million moja, endapo ataendelea kusalia kwenye klabu ya Man utd msimu ujao.
Depay, atakutana na hasara hiyo, kufuatia makubaliano yaliopo katika mkataba wa ongezeko la pesa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Man Utd ambao aliusaini wakati akijiunga na Man utd mwaka 2015 akitokea PSV Eindhoven kwa ada ya uhamisho wa pauni million 25.
Sehemu ya mkataba wa ongezeko la pesa (bonus) kwa wachezaji wa Man Utd, ambayo imevujishwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini England, imeonyesha pesa hiyo atalazimika kuikosa kama Man utd watashindwa kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Kutokana na mwenendo wa klabu hiyo unavyoonekana kwa sasa, kuna wasiwasi wa jambo hilo kujitokeza, kufuatia ushindani mkubwa uliopo katika ligi ya nchini England, ambapo inaonekana Man Utd wana nafasi funyu ya kufaulu kucheza michuano hiyo msimu ujao.
Hata hivyo Man Utd walionyesha matumaini ya kuingia katika nne bora za msimamo wa ligi ya nchini humo, kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata dhidi ya Everton, japo wadadisi wengi wamekua hawatoi nafasi kwa wababe hao wa zamani.
Kwa sasa Depay bado ana mkataba na Man utd hadi mwaka 2018, hali ambayo inadhihirisha changamoto dhidi yake kutokana na mtego uliopo kwenye makubaliano aliyokubaliana na viongozi huko Old Trafford.
Mkataba wa Depay unaonyesha dhahir kiasi cha ongezeko la pesa anastahili kulipata pale Man utd itakapofanya vyema katika michuano ligi ya mabingwa barani ulaya sambamba na michuano mingine, ambapo inaonyesha kama watashinda ligi ya England atapatiwa kiasi cha pauni 2,500,000 na wakimaliza katika nafasi ya pili atapatiwa kiasi cha ongezeko la pauni 1,250,000.
Kwa upande wa ligi ya mabingwa endapo wangechukua angepata 5,250,000, washindi wa pili 2,750,000, hatua ya nusu fainali 1,250,000 na robo fainali 500,000.
Michuano ya Europa League kama Man Utd wangetwaa ubingwa Depay angechukua ongezeko la pesa pauni 1,000,000 na mshindi wa pili angechukua 500,000 huku michuano ya kombe la FA kama Man Utd watachukua ubingwa atapata kiasi cha pauni 1,000,000 na mshindi wa pili atachukua 500,000.
Kombe la ligi (Capital One Cup) endapo Man utd wangetwaa ubingwa angepata paun 500,000 na mshindi wa pili angechukua 250,000.
Mbali na Depay, pia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza ambao wataendelea na mikataba yao kwa msimu ujao wa ligi, watapoteza bahati hiyo hususan katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo kunaonekana ndipo kwenye ongezeko fedha nyingi
0 comments:
Post a Comment