Kiongozi wa chama cha Conservative cha Ujerumani Andreas Scheuer amependekeza kuwa kijerumani kitumike wakati wa salah misikitini nchini humo badala ya Kiarabu.
Mwanasiasa huyo aidha anasema kuwa ni sharti Ujerumani izuie ufadhili wa misikiti kutoka Saudi Arabia na Uturuki.
Katibu huyo mkuu wa chama hicho cha CSU ambacho ni mshirika wa chama kinachoongozwa na Kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel cha CDU analaumu siasa za kiislamu kwa kuhujumu mtagusano baiana ya Wajerumani waislamu na wakristo.
Maimamu wanaoendesha swala na misikiti nchini Ujerumani wanapaswa kujifunzia hukohuko Ukerumani wala sio Arabuni
Maoni yake yanawadia huku kukiwa na mtafaruk mkubwa wa kidiplomasia baina ya Ujerumani na Uturuki kuhusiana na uhuru wa kujieleza.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasilisha mahakamani kesi dhidi ya mchekeshaji mjerumani Jan Boehmermann.
Rais huyo anadai kuwa Boehmermann alimkosoa heshima katika moja ya mashairi yake iliyopeperushwa na runinga ya taifa ZDF.
Inadaiwa kuwa mchekeshaji huyo nguli aliwatahadharisha watazamaji kuwa atakachokisema kitakiuka haki za kujieleza za wajerumani kabla kumtusi rais Erdogan.
Jan alisema kuwa Erdogan hushiriki ngono na wanyama kama vile mbuzi na kondoo.
Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wangali wanachunguza tukio hilo ilikubaini iwapo msanii huyo nguli atashtakiwa kwa kumkejeli na kumtusi rais wa taifa la kigeni.
Serikali ya Uturuki ilisajili kesi hiyo rasmi kw balozi wa Ujerumani nchini humo mjini Ankara.
Hilo ndilo tukio la pili ambalo linaonekana kuikasirisha sana Ankara.
Awali wimbo mmoja uliopeperushwa kwenye runinga inadaiwa kuukejeli uongozi wa bw Erdogan.
Mchekeshaji huyo amepewa ulinzi mkali wa polisi na hata shoo yake ijayo imepigwa marufuku.
Kesi hiyo imemweka pabaya Kansela wa Ujerumani bi Merkel kwani yeye pamoja na viongozi wenza wa bara Ulaya wanaisihi Uturuki(Erdogan) kutekeleza upande wao wa makubaliano ya kusitisha wimbi la wahamiaji kutoka Syria.
0 comments:
Post a Comment