Mmiliki wa gazeti la Daily Mail yuko katika mashauriano na pande zingine katika mikakati ya kuinunua kampuni inayokumbwa na matatizo ya Marekani Yahoo.
Msemaji wa kampuni hiyo amesema majadiliano yako katika awamu za kwanza kwanza na hakuna uhakika kuwa makubaliano yatapatikana.
Jarida la Wall Street , ambapo mikakati hiyo ilitangazwa kwanza , limesema kuwa gazeti la Daily Mail na General Trust walikuwa wakijadiliana kuhusu ununuzi huo pamoja na makampuni mengine ya kibinafsi.
Kampuni ya Yahoo iko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa wanahisa kuitaka kujiimarisha .
Mwenye hisa nyingi zaidi kwenye Yahoo hivi majuzi alisema kuwa bodi nzima inastahili kubadilishwa kutokana na hasara ya kampuni hiyo.
Msemaji wa Daily Mail amesema, wakizingatia mafanikio ya Dailymail.com na Elite Daily, wamekuwa katika majadiliano na pande tofauti ambazo zina nia ya kuinunua Yahoo.
0 comments:
Post a Comment