Mamia ya ng'ombe na fahali walitembea kwenye
jukwaa mwishoni mwa juma katika mji uliopo kaskazini mwa India Rohtak
katika maonyesho ya aina yake ya urembo.
Hafla hiyo iliandaliwa na serikali ya eneo hilo kutoa mafunzo kuhusu aina tofauati za ng'ombe na haki za mifugo hao. Zaidi ya ng'ombe 600 na fahali walishiriki na mmiliki ng'ombe aliyeshinda alijinyakuliwa zawadi ya dola 3,600. Wakulima waliwasili na mifugo yao kutoka wilaya za
jimbo la Haryana na waliona fahari wakati ngo'mbe na fahali wao
walipotembea juu ya jukwaa. Huku wengine wakitembea bila matataizo na kwa madaha wengine walibidi kusukumwa ili wamalize. Mafahali walikaguliwa kwa uzito, sura na ukubwa wa
pembe zao. Na ng'ombe walikaguliwa kutokana na uzuri wao na uwezo wao wa
kutoa maziwa. Waziri wa kilimo wa Haryana, OP Dhankar, alimtuza mmiliki ng'ombe aliyeshinda.
Wanafunzi
wa taasisi ya kimataifa ya elimu na utafiti wa mifugo sehemu ambako
maonyesho hayo yalifanyika, walipiga picha na ng'ombe walioshinda.
0 comments:
Post a Comment