WhatsApp ina tabia ya kuingiza vitu vipya kimya kimya bila hata mtumiaji kugundua kabisa.
Mpaka sasa wamekwisha boresha vitu vingi sana na vyote vimekua vina umuhimu kwa namna moja au nyingine hivyo basi ni muhimu kuvitambua.  Hebu tufundishane hapa vitu vipya na vilivyokuwepo kwa muda kidogo
  1. bold, italics na strikethrough meseji zako unazotuma.

Hii ni kwa ajili ya kuwekea msisitizo kwenye jambo lakini kwa njia ambayo humkwazi unayemtumia ujumbe kama ambavyo ingekua ukimtumia mtu meseji kwa herufi kubwa.  Na vile vile unaweza kurembesha sehemu ya meseji yako unayotaka kutuma kama kwa kuiweka kwa Italic.
IMG-20160623-WA0051
Pia unaweza ukataka kuelezea kitu ambacho kina makali sana lakini unahitaji ujumbe umfikie muhusika, whatsapp wamesaidia na kwa hilo pia kwa kutuwekea strikethrough
Kwa ku-bold, ongeza * kabla ya neno unalotaka andika na vile vile baada ya neno, ambapo itatokea kama *mambo* unapoandika. Kwa italicize, ongeza _ kabla ya neno unalotaka andika na vile vile baada ya neno _, ambapo itatokea kama hivi _mambo_ na mwisho kabisa strikethrough, kwa hii ongeza ~ kabla ya neno unalotaka andika na vile vile baada ya neno pia na itatokea hivi ~mambo ~.
Lakini pia, unaweza ukafanya vyote hivyo kwenye sentensi moja au neno moja. Kwa kuweka hivyo alama zote kwa pamoja *_ ~ikifuatiwa na neno na kumaliziwa kwa kinyume cha mtiririko uliotumia mwanzoni ~­_*.
IMG-20160623-WA0050

2. Kutuma faili (PDF) kwa watu

Hili kwa sasa sio jipya sana, limekuwepo kwa muda kidogo ila ni vizuri tukashare na wengine ambao hawakua wanajua wajue. Kipengele hiki kinakusaidia kutuma mafile kwa watumiaji wengine wa WhatsApp walioboresha (updates) kwenye version mpya la sivyo utapata taarifa itakayosema faili limeshindwa kwenda kwa mtumiaji huyo.
send-files-via-WhatsApp-pdf-word-excel
Kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android, gusa sehemu ya attachement pale juu kwenye kona ya kulia ya simu yako. Kisha gusa tena sehemu iliyoandika ‘Document’ na hapo sasa unaweza tuma faili lolote kwa watu wako.

3. Unaweza kuweka kumbukumbu ya ujumbe kwa kubonyeza nyota (star).

Mara nyingine katika kuchat, unawezakutumiwa vitu muhimu kama anuani, jina la sehemu unayotakiwa kuenda, na kama tunavyojua chats ni ndefu sana, wengine hata huwa hatufuti chats miezi na miezi. WhatsApp wametuletea kipengele kipya ambapo sasa unaweza ukahifadhi vitu muhimu katika chats zako. Ikifika muda unahitaji kumbukumbu unaingia haraka kwenye meseji zilikua ulizoziwekea nyota (starred messages). Ni rahisi sana kupata unachikitafuta kuliko kukaa unafuatilia ni lini na saa ngapi ulitumiwa kitu unachokita.
whatsapp-starred-messages-5
Gusa kwa muda kidogo kwenye ujumbe unaotaka kuiweka katika kumbukumbu au kuiwekea nyota, kwa juu vipengele vitatokea kasha chagua nyota kwa kuigusa.kuitafuta tena, utaingia settings > starred messegaes. Na hii sio lazima uingie katika chat yako na yule mtu aliekutumia, ukiingia tu moja kwa moja unaipata kwenye settings.
Na ukilizoea hili, utafikia wakati ukiingia sehemu ya meseji zilizokua starred zinakua nyingi, kiasi unaanza kujiuliza ipi ni ipi na inahusu nini, basi ukigusa tu kwenye meseji unayotaka itakurudisha moja kwa moja kwenye chat yako na yule mtu kwa kujikumbusha zaidi.

 4. Kutumia Whatsapp kwenye tovuti.

WhatsApp kwenye tovuti imekua ni kitu kizuri sana tangu kianzishwe. Wanaotumia simu zenye mfumo wa Android wao wamefurahia sana hiki kipengele kwa muda mrefu kuliko watu wanaotumia iPhones.
Screen_Shot_2015-01-21_at_1.21.46_PM.0
Ingia kwenye sehemu ya Settings > Whatsapp web na wakati huo huo kwenye kompyuta yako umeingia kwenye tovuti  web.whatsapp.com kisha pitisha code inayotokea kwenye kompyuta yako kwenye simu yako ‘scanning the bar code’ na hapo hapo anza kuchat na watu wako kwa kutumia kompyuta yako bila kushusha chochote.
  1. Kuweka kumbukumbu ya kuonyesha ‘Visual Reminder’.

Kwa wenye ile tabia unasoma meseji alafu unasema utaijibu badae, alafu unasahau. Hii ni njia nyepesi ya kukufanya ukumbuke kiurahisi. Inakusaidia kuiachia alama ya kijani au blue ili ujue baadae kwamba unatakiwa kuifanyia kazi.  Ukifungua Chat, ukaifunga, gusa kwa muda kidogo au wenye iPhone waswap  upande wa kulia alafu juu kutatokea machanguo kisha chagua ‘mark as unread’ na ukimalizana nayo itajifuta ile rangi ya doti ya kijani au kwa iphone utaiswap tena.
  1. Vitiki vya bluu na Read receipt

Vitiki vya bluu viliwekwa muda kidogo pia, ambapo vinamaanisha uliemtumia ujumbe amepokea na kuusoma. Saa nyingine unahitaji tu kuiangalia meseji ukae chini utafakari cha kujibu ndio umjubu mtu alietuma hata masaa 5 badae, vitiki vya bluu vilitoa uhuru huo. Lakini kwa sasa unaweza ukavitoa na kubakia na vya rangi ya kijivu pekee kwa kuzima ‘Read Recepts.”
Whatsapp-01-GQ-06Nov14_b_813x494
Jua kwamba, kwa kuzima read recept na vijiti vya bluu na wewe pia hutaweza kujua kama meseji zako zimesomwa ala. Lakini kwa meseji za vikundi bado utaendelea kuona kama ujumbe wako umesemwa na wanakikundi. Kwa hivyo ni kukubaliana na hali ilivyo.
  1. Kuweka njia fupi za chats. Shortcuts to conversations

Kama una watu unawasiliana nao mara kwa mara, itakua ni vizuri ukajirahisishia tu ukaweka shortcut ya maongezi yenu kwenye ukurasa wa juu wa simu yako ‘homescreen’ ili usiwe unafungua fungua whatsapp kila saa ili kuongea na huyo mtu mmoja pekee.
stepsix
Gusa kwa muda kidogo chat, labda ni kikundi au mtu mmoja unayeamua we mwenyewe kisha utapata machaguo za kuchagua alafu gusa ‘add conversation shortcuts’. Na mpaka sasa ni kwa watuamiji wa Android pekee.
  1. Jibu moja kwa moja kwa Pop up

Ujumbe mpya ikiingia kwa sasa moja kwa moja kwenye simu yako, sasa sio lazima kufungua whatsapp ila unaweza kumjibu papo hapo. Ingia Settings > Notifications > Popup Notification, na chagua hapo unachopenda na unaweza badili kwa chats zote, za watu binafsi na za vikundi.
IMG-20160623-WA0052

9. Sitisha picha kujipakua zenyewe katika simu yako.

Nafasi kubwa kwenye simu ni muhimu sana, na whatsapp humaliza nafasi kubwa sana, kuzuia hili ingia settings > Privacy > Photos kisha gusa sehemu itakayofanya WhataApp isihifadhi picha kwenye camera roll, japo utaweza kuzishusha (download) kama kawaida utakapoamua ili usikose matukio muhimu.
KPJeNBSe-media-auto
  1. Uwezo wa kurekodi video papo hapo na kutuma

Mwanzoni atumiaji wa mtandao huu waliweza kutuma picha peke yake. Lakini sasa tumeletewa uwezo wa kurekodi na kutuma video papo hapo kwenye chat, haina haja tena ya kuingia sehemu ya video katika simu yako kisha usambaze kwa kupitia whatsapp.
Gusa sehemu ya camera panapotumika kuandikia ujumbe, kisha gusa moja kwa moja kwenye sehemu ya duara ya kurekodia muda wote unakua ukirekodi. Ukiachia inakua imemaliza kurekodi tayari kwa kutumwa kwa mtu huyo au kikundi hicho.