Mahakama
ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma juu ya habari
iliyoandikwa na gazeti la kila siku la Mwananchi toleo la Jumanne, Julai
12, 2016.
Gazeti
hilo lilichapisha habari ambayo Mwandishi wa habari hiyo alimnukuu
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati
akiwataka watendaji wa mahakama nchini kujenga utamaduni wa kuwajibika
na kutoruhusu uhuru wa mahakama kuingiliwa na watu kutoka nje ya
Mahakama.
Kutokana
na habari hiyo, Mahakama ya Tanzania inakanusha taarifa hiyo kwa kuwa
ililenga katika kuipotosha jamii na kuleta msuguano kati ya Mahakama na
Taasisi nyingine.
Ufafanuzi wa Taarifa Hiyo
Mahakama
ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi wa alichokisema Msajili Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mpango Mkakati
wa Mahakama ya Tanzania Jumatatu Julai 11, 2016 mjini Dodoma.
Aidha,
Msajili aliwataka watumishi wa mahakama nchini kutekeleza mpango
mkakati kwa nia thabiti na siyo kuutumia uhuru wa mahakama vibaya
kufunika maovu, badala yake aliwataka wale wenye kasoro katika utendaji
wa kazi kujirekebisha wao wenyewe ndani ya mahakama la sivyo
watarekebishwa hata kutokea nje kwani jamii yetu kwa sasa imedhamiria
kubadilika na haitavumilia utendaji mbovu kwa kigezo cha uhuru wa
mahakama.
Mahakama
ya Tanzania inapenda kuujulisha umma kuwa inafanya kazi na watu wote na
wadau wote nchini ili kuhakikisha nchi inaenda inavyotakiwa na
haitaogopa kukosolewa kinyume na picha iliyopelekwa kwa jamii na habari
iliyopotoshwa kwenye gazeti la Mwananchi.
Mahakama
inashauri waandishi wa habari kuwasiliana na Mahakama endapo kuna jambo
lolote linalohitaji ufafanuzi. Makosa mengine katika taarifa ni kama
vile kukosea cheo kwa kusema Jaji badala ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania na kuandika taarifa kuhusu hatua zinazochuliwa kwa Wahe. Majaji
waliohusika na sakata la ESCEOW ambapo kiukweli katika mkutano huu
halikuongelewa kabisa.
0 comments:
Post a Comment