Siku nane zilizopita, Cristiano Ronaldo alinyanyua ndoo ya Euro 2016 kunako dimba la Stade de France nchini Ufaransa, pale timu yake ya Ureno ilipowabwaga Ufaransa ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Baada ya kucheza kwa takriban dakika 25 tu kabla ya kutolewa nje kufuatiwa kuumizwa goti na Dimitri Payet, kulikuwa na tetesi kuwa jeraha hilo lingemweka nje ya uwanja kwa miezi minne mpaka mitano.
Jana Jumatatu, gazeti la Marca limetoa taarifa mpya juu Ronaldo na inaoekana kwamba, atakuwa nje kwa mwezi mmoja tu mpaka baada ya mapumziko mafupi ya awali kupisha michezo ya kimataifa.
Ronaldo ataukosa mchezo wa European Super Cup
Kama ilivyoripotiwa, Cristiano Ronaldo atakosa mechi za pre-season vilevile mchezo wa European Super Cup dhidi ya Sevilla utakaopigwa Agosti, 2016.
Ligi ya Uhispania maarufu kama La Liga itaanza kutimua vumbi August 21 ambapo Real Madrid watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Real Sociedad kabla ya kukutana tena na Celta Vigo wiki itakayofuata.
Ronaldo ataikosa michezo yote hiyo kutokana na kupewa mapumziko hayo huu akiuguza jeraha lake huko Ibiza.
Je, anarejea lini?
Ronaldo atarejea Septemba 11 ambapo mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Osasuna
Mchezo huo dhidi ya wabishi hao waliopanda daraja msimu huu utapigwa kunako dimba la Bernabeu.
Hii ina maana kwamba Ronaldo atakosa michezo miwili kwenye timu yake ya taifa, mmoja ukiwa ni wa kirafiki na mwingine wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uswizi.
0 comments:
Post a Comment