https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    NI KUFA AU KUPONA FAINALI YA EURO 2016, URENO VS UFARANSA, JE, RONALDO KUVUNJA REKODI YA PLATINI LEO?


    Portugal v France
    Na Mahmoud Rajab
    Michuano ya Euro mwaka huu inayofanyika nchini Ufaransa ndiyo inafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ureno na wenyeji Ufaransa utakaofanyika katika uwanja wa Stade de France uliopo kitongoji cha St. Saint-Denis jijini Paris majira ya saa nne za usiku.
    Taarifa muhimu za kila timu.
    Beki wa Ureno Pepe anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya paja.
    Kocha wa Ureno Fernando Santos anaweza kuamua nani wa kumuanzisha kati ya Danilo au William Carvalho, ambaye amemaliza adhabu yake ya kukosa mchezo mmoja.
    Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kwa mara nyingine tena atakuwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 23 pasipo na majeruhi hata mmoja.
    Atakuwa na mtihani mzito ama amrudisha kiungo N’Golo Kante au aendelee kumtumia Moussa Sissoko.
    Uchambuzi kuelekea mchezo wa leo.
    Wakiwa kama wenyeji wa mashindano, Ufaransa watakuwa na kibarua kizito mbele ya wabishi wa Ureno ambao wamefika hatua hii kwa mbinde mno.
    Ufaransa wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa siku ya leo, kwani itakukmbuka tu mwaka 2004 wakati huo Ureno walipoandaa mashindano haya walijikuta wakiukosa ubingwa nyumbani baada ya kufingwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Ugiriki.
    Kocha  wa Ureno Fernando Santos tangu awali amedai kuwa timu yake haikuwa ikicheza soka safi lakini wangefika hatua hii ya fainali na ama hakika wamefanikiwa kufika.
    Hata hivyo, Ufaransa wamekuwa hatari mno, mpaka sasa wakiwa wameweka kimiani mabao 13. Bao moja zaidi katika mchezo wa leo litawafanya waifikie rekodi ya mabao mengi katika msimu mmoja wa Mashindano ya Ulaya ilyiwekwa na wao wenyewe mwaka 1984.
    Mshambuliaji Antoine Griezmann amekuwa msaada mkubwa kwenye timu hiyo mpaka sasa akiwa na magoli sita na kukinyemelea kiatu cha dhahabu. Ndiye aliyefunga magoli mawili ya ushindi dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali.
    Deschamps amesema kwamba kufika kwao fainali kutasaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha faraja kwa watu nchini humo hasa baada kumbukumbu mbaya ya mauaji ya watu 130 yaliyotokea Novemba mwaka jana kutokana na shambulizi la kigaidi.
    “Hatuna nguvu ya kutatua matatizo ya watu wote wa Ufaransa lakini tunaweza kupunguza wasiwasi wao,” amesema Deschamps.
    “Wachezaji wanafahamu fika uwepo wa nguvu hiyo na kitu na pekee ambacho wanaweza kufanya ni kuvaa kiuhakika rangi ya jezi hizi. Unapoona mwamko na hisia kubwa ndani na nje ya uwanja. Timu hii ina kila sasbabu ya kupendwa, wachezaji wanacheza katika kiwango bora uwanjani na ama hakika ninafarijika sana.”
    Takwimu za michezo waliyokutana
    • Ufaransa wameshinda michezo yao 10 iliyopita dhidi ya Ureno. Rekodi ya jumla ni; Ufaransa wameshinda mara 18, sare 1, na kufungwa mara moja.
    • Mara ya mwisho Ureno kuzuia kipigo kutoka kwa Ufaransa ilikuwa ni mwaka 1975, wakati waliposhinda 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jijini Paris.
    • Ushindi wa Ufaransa kwenye michezo 10 dhidi ya Ureno unajumuisha hadi michezo  mitatu ya kwenye mashindamo makubwa, yote imekuja katika hatua ya nusu fainali. Michel Platini alifunga goli la ushindi kwenye mchezo ulioisha kwa matokeo ya 3-2 kweye Euro mwaka 84, wakati huo huo Zidane alifunga goli muhimu kwa njia ya penati katika ushindi wa mabao 2-1 kwenye Euro mwaka 2000. Na kwa mara nyingine tena Zidane alifunga kwa mkwaju wa penati na kuwapeleka Ufaransa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006 baada ya kushinda goli 1-0.
    • Timu hizi mbili zimekutana mara mbili kwenye michezo ya kirafiki ndani ya miaka miwili. Ufaransa maarufu kwa jina la Les Bleus walishinda mabao 2-1 kwenye uwanja wa Stade de France October mwaka 2014, magoli yakifungwa na Paul Pogba na Karim Benzema huku la Ureno likifungwa na Ricardo Quaresma kwa mkwaju wa penati. Mchezo mwingine uliochezwa Septemba jijini Lisbon mwaka jana ulishuhudia Ufaransa wakishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Ricardo Quaresma kwa mpira wa adhabu ndogo.
    Ureno
    • Ureno wamecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya michuano hii bila ya kubeba taji (michezo 34 kabla ya fainali ya leo). Kama wakiwafunga Ufaransa basi rekodi hii mbovu itaangukia kwa England ambao wamecheza michezo 31.
    • Ndiyo timu ya kwanza kufika hatua ya fainali baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi. Kabla ya hapo imeshawahi kutokea mara mbili tu kwenye Kombe la Dunia lakini Argentina (mwaka 1990) na Italy (mwaka 1994) walimaliza katika nafasi ya pili.
    • Ureno hawajafungwa kwenye michezo yao 13 iliyopita ya kimashindano chini ya kocha Fernando Santos  huku ushindi wao kwenye michezo nane kati ya hiyo walishinda kwa tofauti ya goli moja-moja.
    • Cristiano Ronaldo ameshindwa kufunga goli kwenye mipira yote ya adhabu ndogo ambayo amewahi kupiga akiwa na Ureno. Amepiga free-kicks 43.
    • Magoli yake yote kwenye michuano hii, yamefungwa ndani ya eneo la penati. Matano kati ya hayo ymefungwa kwa kichwa.
    Ufaransa.
    • Ufaransa wameshinda fainali tatu kati ya nne za Kombe la Dunia na Euro. Wakati pekee ambao walimaliza nafasi ya piliilikuwa ni kwenye Kombe la Dunia mwaka 2006. Walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Italy na baadaye kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
    • Hawajafungwa kwenye michezo yao 18 ya Kombe la Dunia na Michuano ya Euro waliyocheza kwenye ardhi yao ya nyumbani, wakiwa wameshinda mara 16 na kutoa sare mara 2. Mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni mwaka 1960 kwenye uzinduzi wa Michuano ya Ulaya (walipoteza michezo yao yote miwili, nusu fainali dhidi ya Yugoslavia na mshindi wa tatu dhidi ya Czechoslovakia).
    • Ushindi katika mchezo wa leo utawapelekea kuungana na Ujerumani na Uhispania kuwa wamenyakua ndoo hii mara tatu.
    • Kati ya magoli yote 13 ya Ufaransa kwenye michuano hii, magoli 11 yamefungwa kuanzia dakika ya 42 kuendelea.
    • Rekodi ya magoli mengi kwenye michuano ya msimu mmoja ya Euro inashikiliwa na Ufaransa (mwaka 1984 walifunga magoli 14).
    • Ufaransa ndio timu ya mwisho kushinda Ubingwa wa Ulaya baada ya kuanza kufungwa (walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushndi wa mabao 2-1 dhidi ya Italy kweye mchezo wa fainali mwaka 2000).
    • Antoine Griezmann anaweza kuwa mchezaji wa tatu wa Ufaransa kuwa mfungaji bora wa michuano mikubwa ulimwenguni, kufuatia Just Fontaine (kwenye Kombe la Dunia mwaka 1958) na Michel Platini kwenye Euro ya mwaka 84.
    • Didier Deschamps anaweza kuwa kocha wa pili kushinda Mashindano ya Ulaya kama mchezaji na kocha pia, baada ya Berti Vogts wa Ujerumani ambaye alifanya hivyo mwaka 1972 akiwa mchezaji na 1996 akiwa kama kocha.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NI KUFA AU KUPONA FAINALI YA EURO 2016, URENO VS UFARANSA, JE, RONALDO KUVUNJA REKODI YA PLATINI LEO? Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top