Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wadau wa Nishati na Madini(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030 katika viwanja vya mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akionyesha jalida maalum wakati wa uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL)wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030.Kushoto kwake ni Mratibu mkazi wa shirika la umoja wa Mataifa na mwakilishi wa shirika la Maendeleo la Kimataifa Bw.Alvaro Rodrigez (UNDP) na Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika Bi.Tonia Kandiero.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akikata utepe kuzindua mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030 jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mratibu mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa na mwakilishi wa shirika la Maendeleo la Kimataifa(UNDP).
Baadhi ya Wadau mbali mbali wa Nishati na Madini wakimsikiliza Mhe.Prof Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali kutoka Umoja wa Mataifa,Benki ya Maendeleo ya Afrika na Umoja wa Ulaya baada ya uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Prof Sospeter Muhongo amesema kuwa uwekezaji wa umeme Vijijini awamu ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.Waziri Prof. Muhongo ameyasema hayo Leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mpango wa Nishati endelevu kwa wote (SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030.
“Mpango huu umelenga kufanikiwa mwaka 2030, lakini kwa sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na Programu hii italifanya taifa letu lijulikane dunia kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu apate umeme,KWANI utasaidia suala la ajira na kutokomeza umaskini, kwaiyo kama nchi tuko katika ngazi za juu za huu mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali”Alisema Prof Muhongo.
Aidha alisema kuwa Programu hii ya Umoja wa Mataifa itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani inafanana sana na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi kutokana na Gesi,Makaa ya Mawe,Umeme wa maporomoko ya Maji,Umeme wa Jua,Joto Ardhi na Mabaki ya mimea na kwa hivi tutafanikisha kujenga nchi ya viwanda kwa sababu tuna miradi ambayo itahakikisha uwepo wa umeme wa uhakika kwa ajili ya uchumi wa Taifa letu.
Amesema mashirika mengi yamesaidia katika kufanikisha upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo imetoa dola milioni 200, Umoja wa Ulaya umetoa euro 180, Nchi za Nordic zimetoa dola milioni 300 pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika nayo imetoa fedha katika kuwekeza kwenye umeme vijijini pia.
0 comments:
Post a Comment