Kaimu
Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Bw
Alex Nkenyenge (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa
Rock City Marathon wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es jana.
Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya
Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki (wa kwanza
kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund(
FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambao ndio wadhamini wakuu wa
mbiohizo Bw Pratik Patel (wa pili kulia), Bi Ombeni Savara katibu Mkuu
Msaidizi chama cha Riadha Tanzania (wa kwanza kulia) na Joseph Kahama
mwenyekiti wa maandalizi ya mbio hizo.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Joseph Kahama akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mwanaridha mkongwe nchini Bw Juma Ikangaa akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund (FCF) na African
Wildlife Trust (AWT), ambae ndio wadhamini wakuu wa mbio
Kaimu
Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Bw
Alex Nkenyenge akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rock City Marathon.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.
Rock
City Marathon ilizinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam huku wito
ukitolewa kwa wadau wa mchezo wa riadha kote nchini kuhakikisha
wanafanya jitihada za makusudi kuukomboa mchezo huo uliolipa taifa
heshima miaka ya nyuma.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mbio hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa na
Michezo Bw Nape Nnauye, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo wa Wizara
hiyo Bw Alex Nkenyenge alisema kuna haja ya kuwepo kwa jitihada za
makusudi miongoni mwa wadau wa mchezo huo ili kurejesha makali ya taifa
katika riadha yaliyoonyeshwa miaka ya 1970 na 1980.
Kupitia
mkurugenzi huyo Waziri Nape alitoa wito kwa wadau wa mchezo huo
kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhakikisha changamoto
zinazokwamisha mchezo huo zinatatuliwa ili kuwezesha uwepo wa maandalizi
ya kutosha kwa wanamchezo huo.“Ndio maana nawapongeza waandaaji wa mbio
hizi kwa kuwa wanashikiri moja kwa moja kukamilisha adhma yetu hii
muhimu…kama serikali pia tunaahidi kuendelea kushirikiana nao,’’
alisema.
Akizungumza
kwenye hafla Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus
International, Bi Elizabeth Riziki alisema mbio hizo zinatarajiwa
kufanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza zikihusisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo baadhi
ya nchi za Afrika, Ulaya na Marekani. Alisema mbio hizo zinazofanyika
kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinalenga kutambua na
kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani
kupitia sekta ya michezo.
“Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, mbio za kilomita 3 kwa ajili ya walemavu, mbio za kilomita 3 tena kwa ajili ya wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na mbio za kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19,’’ alitaja.
Alitaja baadhi ya makampuni yaliyojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited na kampuni ya Real PR Solution.
“ Pia mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuwa zitaambatana na uwepo wa majiko ya wachoma nyama ili kutoa fursa kwa washiriki kufurahia aina hiyo ya kitoweo pamoja na vyakula tofauti vyenye asili ya mkoa huo…ifahamike lengo la mbio hizi kukuza utalii wa ndani ,’’
Tunawaalika
wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka
huu kuwa bora zaidi,” alisema.Akizungumza kwenye hafla hiyo mdhamini
mkuu wa mbio hizo Bw Pratik Patel ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa
mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust
(AWT) alisema wameamua kuwa sehemu ya mbio hizo kwa kuwa zinaendana na
mkakati wao kukuza utalii kwa kulinda maliasili.
“Tunafurahia kuwa sehemu yam bio hizi kwa kuwa lengo lake linaenda sambamba na agenda yetu ya kulinda maliasili na zaidi linaenda sambamba na kampeni yetu ya kupinga vita ujangili inayofahamika kama ‘Okoa Wanyama Wetu; Kataa Ujangili’. Alisema.


0 comments:
Post a Comment