Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) amekamatwa na polisi akiwa
nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro
amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge
huyo.
Jana
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa
Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa
ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
Waliokamatwa
na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally
Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi,
Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa
mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand
Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini
walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti
kituoni hapo leo Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment