Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
Mwezeshaji Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Baadi ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza. Na Mwandishi wetu
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazoendelea kuibuliwa.
Kauli hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania, Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini Mwanza.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750 kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.
Katika kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe mkombozi wa maisha yao.
Akizungumza katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo, lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma hivyo kuchangia kiasi kidogo katika kumuendeleza mkulima.
“Kwa kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,” alisema Dk Kida
Alisema kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.
Katika warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda (Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na ufugaji wa samaki na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa mpya za kilimo biashara.
Alisema kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa kilimo lazima kiwe vijijini.
Alisema ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea teknolojia ya kisasa katika wilaya za Bunda, Bukoba vijijini, Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa kipindi cha miaka mitatu.
Pamoja na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha hiyo.
Akifungua kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko sekta nyingine duniani kote.
Mongela aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa tafiti hizo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.
Licha ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi hiyo.
“Hizi tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella
Amoni Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.
Katika kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP ikishirikiana na ESRF.
0 comments:
Post a Comment