Na Beatrice Lyimo, Maelezo
Serikali inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania
Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa
blog nchini.
Waziri
Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania
kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi
ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha,
Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo
na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo
ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo
hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo
makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo
yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie
fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha
tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma
mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua
Waziri Nape.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi
wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja
na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri
Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania
kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi
ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza
mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers
Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa
waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.
Mmoja
wa Wajumbe wa mkutano huo,Mzee John Kitime ambaye amebobea katika mambo
ya Hakimiliki,akitoa elimu ya mambo ya Hakimiliki kwa washiriki wa
mkutano huo.
Baadhi ya Wadau wakiendelea kusikiliza yaliyokuwa yakiendelea ukumbini humo.
Mmoja wa wajumbe Daniel Mbega akiuliza swali wakati wa mkutano huo ulipokuwa ukiendelea
Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea
Mwenyekiti
wa Muda wa chama cha Waendesha mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers
Network-TBN,Joachim Mushi akimkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kufunga mkutano
huo na pia kuyotolea ufafanuzi baadhi ya mambo.
Baadhi ya Waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa kwenye mkutano wao wa Mwaka wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea
0 comments:
Post a Comment