https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MADAI YA KUBEBA UNGA: RAY C AJISALIMISHA POLISI

    BAADA ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ na baadaye ‘kustaafu’, madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ‘msala’ ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa hiari yake, bila kusukumwa ajisalimishe polisi.
    Msanii wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ akiwa Hospitali ya Mwananyamala .
    Hivi karibuni, Ray C alijikuta akiangua kilio ndani ya Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar baada ya kuhusishwa na ishu ya uuzaji wa unga.
    Kwa mujibu wa chanzo chetu, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alidai alishtukiwa na mtu wa intelejensia (usalama wa taifa) ambaye amekuwa akimfuatilia kutoka nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar anakoishi kwa sasa.
    KAWE DARAJANI
    Chanzo hicho kilinyetisha gazeti la Ijumaa Wikienda kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na ‘kumbloku’ kwa mbele.
    Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI.
    Ray C katika pozi.
    Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi.
    Ray C alimua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi.
    LUGALO
    Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo alisimama na jamaa huyo aliyekuwa akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na kumtaka Ray C ashuke ndani ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia kuwa alikuwa amebeba unga.
    Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alitoa kitambulisha kuwa yeye ni askari.
    Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.
    ‘Ray C’akiingia kwenye gari lake aina ya 'Toyota Carina'.
    MAELEWANO YASHINDIKANA
    Baada ya kuona hivyo, Ray C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay lakini jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo Ray C alishindwa kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia waambatane hadi kituo kidogo cha  Polisi cha Mwenge.
    Jamaa huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa kasi na kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na alipoona wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo.
    Ilisemekana kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku akiangua kilio.
    Taarifa zilidai kwamba jamaa huyo aliendelea kumfukuzia Ray C hadi Mabatini ambapo yeye alibana nje wakati Ray C akiwa kwa mkuu wa kituo.
    Hata hivyo, baadaye jamaa huyo naye alijisalimisha kwa mkuu wa kituo ambapo naye alijieleza kwamba aliambiwa na watu wa usalama kuwa afuatilie gari hilo lililohisiwa kubeba unga.
    Ilielezwa kwamba mkuu huyo wa kituo ameamuru jamaa huyo kuchunguzwa ili kubaini malalamiko ya Ray C.
    Mwanadada kiuno bila mfupa 'Ray C'.
    BOFYA HAPA KUMSIKIA RAY C
    Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima.

    Alifunguka: “Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge baada ya kufika kwenye Makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na trafiki akiwa pembeni nikawasimamisha na kuwaeleza.
    “Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.
    “Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi.
    “Baada ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume nikaongozana nao hadi katika gari langu na kupekuwa kila sehemu lakini wakasema hapakuwa na chochote kibaya, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa kituo akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda Mwananyamala hospitali kumeza dawa.
    “Kama kweli alikuwa ni mtu wa usalama au askari, alitakiwa kuvaa sare na kufuata utaratibu wa kunipekua na siyo kunikimbiza kwani nilijua ni jambazi.
    “Nusura nife kwa presha kwani nilijua ni mtu mbaya tu anataka kunidhuru afya yangu, lakini namshukuru Mungu sikupaniki zaidi ya kulia. Hata hivyo mkuu wa kituo ameahidi kulishughulikia suala hilo kwa kufanya uchunguzi baada ya jamaa huyo naye kujisalimisha polisi.”
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MADAI YA KUBEBA UNGA: RAY C AJISALIMISHA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top