Umdhaniaye siye ndiye. Michuano
ya Kombe la chama cha soka cha Uingereza, FA, hatua ya nne (4) imeacha
mshituko mkubwa pale vilabu vilivyopewa nafasi vilipofungashwa vilago na
wale ambao awali walioonekana kama ‘vibonde’
Chelsea 2 Bradford City 4, kwa
umakini mkubwa klabu ya Bradford ilifanikiwa kurejesha goli mbili za
haraka kutoka kwa Gary Cahil na Mbrazil, Ramires upande wa Chelsea na
hivyo kuwang’oa vinara hao wa ligi kuu katika michuano hiyo tena katika
dimba lao la ‘darajani’ Stamford Bridge.
City wanashiriki ligi daraja la
kwanza na mpaka dakika ya 38, walishakuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini
walipambana vilivyo na kufuzu kwa raundi ya 5 ya michuano hiyo na hivyo
kuzima ndoto ya vikombe vinne upande wa Chelsea msimu huu.
Chelsea reject Filipe Morais
levelled the fourth-round tie with 15 minutes to go before Jon Stead,
the scorer of City’s first, teed up Andy Halliday for the winner eight
minutes from time.
And substitute Mark Yeates tucked
in a stoppage-time fourth to inflict the Blues’ first home loss this
season and spark jubilant celebrations from Phil Parkinson’s visitors.
Manchester City 0 Middlesbrough
2, goli toka kwa nyota wa chelsea aliye kwa mkopo Patrick Bamford pamoja
na shuti la Kike yalitosha kuiwezesha klabu inayowania kupanda ligi kuu
ya Middlesbrough kuwashitua na kuwashangaza mabinghwa wa tetezi wa
taji la ligi kuu pale yalipowatupa nje kunako michuano ya FA
Nyota huyo toka uingereza
alitumiia vyema udhaifu wa safu ya ulinzi kabla ya Kike kuingia na
kufunga akitokea benchi katika dakika za majeruhi dimbani Etihad ambapo
siyo rahisi kuondoka na alama tatu kwa vilabu vingi
City walitawala mchezo huo kunako
kipindi cha kwanza lakini hata hivyo mlinda lango wa zamani wa miamba
ya hispania anyecheza Boro, Tomas Mejias alikuwa kikwazo. Na kama vile
haitoshi mpira ulopigwa na Frank Lampard uliguswa na kugonga mwamba
dakika ya 89 kabla Kike hajawaadhibu kwa goli la pili.
Southampton 2 Crystal Palace 3,
ni mchezo ambao ulishuhudia jumla ya mabao matano yakifungwa huku
ikishuhudiwa vijana wa meneja wa zamani wa Newcastle Alan Pardew
wakitoka nyuma na kuwafunga ‘Saints’walio katika ubora wao.
Awali, Graziano Pelle aliifungia
“saints’ dakika ya tisa bao ambalo halikudumu kwani lilisawazishwa na
mfaransa aliyepata kukipiga Arsenal Marouane Chamakh mda mfupi baadaye.
Kisha baada ya mlinzi Scott Dann kujifunga, Palace wakasawazisha tena
ndani ya dakika tano kupitia kwake nyota mwingine wa Arsenal aliye kwa
mkopo klabuni hapo Yaya Sanogo. Baadaye Chamakh akatikisa tena wavu kwa
mara ya pili na kuivusha klabu hiyo kwa hatua inayofuata
Blackburn Rovers 3 Swansea City
1, miamba mingine ya ligi kuu iliyong’olewa kunako FA ni swansea pale
mchezaji ambae taarifa zinadai anawaniwa sana na vilabun vya ligi kuu
Rudy Gestede alipofunga bao maridhawa kwa upande wa Blackburn na
kuwawezesha kuwatoa Swansea waliomaliza pungufu katika pambano hilo kwa
ushindi wa bao 3-1
Awali, mchezaji Kyle Bartley
alitolewa nje kwa kadi nyekundu kunako dakika ya saba tu lakini bado
Gylfi Sigurdsson alifunga bao murua kunako dakika ya 21 na kuiwezesha
swansea kuongoza kwa muda pambano hilo. Iliwachukua dakika mbili tu
Rovers kusawazisha kupitia kwake Chris Taylor na kisha mchezaji
aliyetokea benchi Gestede, aliyepata pia kuichezea Cardiff city
akawatanguliza wenyeji kwa bao la pili zikiwa zimebaki takribani dakika
kumi na mbili (12) pambano limalizike. Bao la tatu lilifungwa naye Craig
Conway kunako dakika ya 89 ya pambano hilo.
Tottenham Hotspur 1 Leicester
City 2; Pamoja na kufunga mapema kupitia mkwaju wa penalti kufuatia
madhambi alofanyiwa mshambulizi, Roberto Soldado bado totenham ilitolewa
katika pambano lingine la kushangaza la mchuano wa kombe la FA. Mkwaju
huo uliwekwa kimiani naye Andros Townsend, lakini haukutosha kwani
mabao toka kwa Leonardo Ulloa na Jeffrey Schlupp yalitosha kuwazima
kabisa wenyeji dimbani kwao, White Hart Lane.
Awali hali ilionekana kuwa mbaya
kwa Leicester kwani siyo tu walifungwa penati hiyo kunako dakika ya 19
lakini pia walishuhudia kunyimwa na penati iliyofuatia na adhabu ya kadi
ya njano kwa usajili wao mpya Andrej Kramaric kwa madai ya kujirusha.
Hata hivyo, zikiwa zimebaki
dakika saba tu, Leonardo Ulloa alifunga bao murua kisha mlinda lango wa
Spurs Vorm akaruhusu mpira wa Schlupp kuvuka msitari na kuwapa leicester
nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.
Katika michzo mingine za raundi
hiyo, Nyota mnaijeria Victor Anichebe alifunga mara 2 ndani ya dakika 10
na kuwasaidia West Brom Albion kuwafunga wapinzani wao wa jadi
Birmingham City 2-1, Sunderland ikatoka suluhu tasa na Fulham katika
pambano ambalo Jack Rodwell alitolewa nje kufuatia kadi mbili za njano.
Timu hizo zitalazimika kurudiana tena kumpata mshindi. Reading nayo
ikaifunga Cardiff 2-1, Derby ikaifunga Chesterfield 2-0 Darren Bent akifunga. Ilihali Preston ikambulia 1-1 dhidi ya Sheffield United. Wakati pambano la usiku Bolton Wanderers iliikomalia Liverpool na kuambulia sare pia.