TUNISIA wanaanza kampeini zao leo
za kusaka ubingwa wa kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2015 kwa
kukabiliana na Cape Verde katika mechi ya kundi B itayopigwa uwanja wa
Nuevo Estadio majira ya 4:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Wakati miamba hiyo ya soka
kaskazini mwa Afrika ikiingia uwanjani kama moja y
a timu inayopewa
nafasi ya kutwaa ubingwa kufuatia kampeini nzuri wakati wa mechi za
kufuzu, Cape Verde wanaingia uwanjani kama wachanga kabisa.
Hata hivyo Cape Verde ‘Blue
Sharks’ ambao wanashiriki kwa mara ya pili Afcon (walishiriki kwa mara
ya kwanza 2013 nchini Afrika kusini na kuonesha kiwango cha juu),
wamekuwa miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa kiwango cha juu kisoka
duniani miaka miwili au mitatu iliyopita.
Mechi ya mapema itayoanza majira ya saa 1:00 usiku inawakutanisha Zambia dhidi ya DR Congo.
MATOKEO YA MECHI ZA JANA KUNDI A
| MECHI | MATOKEO |
| Guinea ya Ikweta v Congo Brazaville | 1 : 1 |
| Burkina Faso v Gabon | 0 : 2 |

