Bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi ya India alifanya maamuzi ya papo kwa
hapo kuolewa na mmoja wa wageni waliofika kushereheka naye katika
harusi yake baada ya mumewe kuugua ghafla.
Mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra anayetokea Rampur jimbo la Uttar
Pradesh, inaelezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya wawili hao mume
akaanguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini na kwenda kumwona
daktari.
Bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume
alimficha juu ya hali yake, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa ,
jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.
Indra akatoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia
ya bwana harusi , ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya
nduguye,na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake, jamaa
akaona nyota ya jaha imemuangukia, si akakubali !
Ndoa ikafungwa, hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha