Mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke Kitengo cha Usafishaji,
Ramadhani Athuman akiweka dawa katika vyombo alivyokuwa akitumia kuhifadhia
kinyesi mwalimu Gaudensia Albert wa Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es
Salaam, kabla vyombo hivyo havijaenda kutupwa dampo. (Picha na Francis Dande)
Umati wa watu ukiwa nje ya nyumba wakati zoezi la kuteketeza kinyesi likiendelea.
Kinyesi kikiwa kimehifadhiwa ndani ya chumba cha mwalimu.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke wakiondoa kinyesi katika nyumba ya mwalimu Gaudensia.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke wakiondoa kinyesi katika nyumba ya mwalimu Gaudensia.
Maulid Liuguyo ambaye ni mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke kitengo cha usafi akishiriki katika zoezi hilo.
Na Mwandishi Wetu
Manispaa
ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika
chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert
baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili
kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.
Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo,
Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na
wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya
wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi
jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye
utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.
“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo
tulischukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama
mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza
kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo.
Alisema pamoja na kuutekeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja
mikojo na matapishi bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo
kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.
“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana
kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi kuamini mambo ya ushirikina lakini
haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na kuhifadhi uchafu kama ule
ndani,”alisema.
Aidha, alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la
tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uwaangalizi wa
polisi.
Tembo, alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo
la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya
Taifa muhimbili kwa ajili ya kupimwa afaya baada ya kupata mshituko ambao
umesababishwa na taarifa hizo.
Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema
uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi
inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.
Pia alisema kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa
kutoka idara mbalimbali kupima uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta
wangemkamata kwa hatua za kimfikisha mahakamani.
Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa
amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza
mahakamani.
“Tukio hili kwa manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yani
inaekekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili za kawaida
asingeweza kufanya na mna hii,”alisema.
Umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi
tangu saa tatu asubuhi wakisubiri kazi hiyo hadi ilipofnyika saa tisa jioni na
wataalamu wa manispaa hiyo.
Wataalamu hao walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza ubeba
na kutumbukiza chooni kwa uangalifu mkubwa.
Walipomaliza walvisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa
ambazo zimeweza kusaidia kuondoa harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.
Awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika
kusimamia kuvujnjwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika
ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.
Tukio hilo ambalo limekuwa likifuatiliwa na majirani
hususan jana wakati wa uteketezaji lilitokea Februari 22 mwaka huu.