Hivi ndivyo Club Olympia ilivyoteketea kwa moto na kusababisha uharibifu wa Mari nyingi na zengine kuibiwa
Mmiliki
wa Club Olympia Bwana Samwel Mwaisumbe akitoa maelezo juu ya Moto
uliounguza Pub yake kwamba inasemekana moto huo ulisababishwa na
Hitilafu ya umeme na kuwa wao hawakuwa na taarifa wakati moto unaanza ni
msamalia mwema tuu majira ya saa kumi na moja alfajiri ndiye alitoa
taarifa kwa jeshi la Zima moto kuwa kuna moto unawaka eneo hilo,
ameongeza kuwa mali nyingi zimeteketea kwa moto na zengine kuibiwa,
alimalizia kuwa hakuna mtu aliyepata madhara kwa sababu wote hawakuwepo
katika pub hiyo.
Mmoja
wa wakuu kutoka kikosi cha zima moto J.K Mwasabeja akielezea juu ya
tukio la moto huo, na kusisitiza taarifa kamili itakuja baadae mara
baada ya uchunguzi kukamilika.
Club Olympia kwa nje
Kikosi cha Askari wa zimamoto wakiwa bado wanaendelea na kazi yao
Lango la Kuingilia Club Olympia
Baadhi ya maeneo ambayo yameteketea
Hili ni eneo ambalo limepona na Moto
Eneo la ndani ya Club hiyo
Eneo la Counter
Eneo la Jikoni
Eneo la watu ambapo watu walikuwa wakikaa
Baadhi ya watu wakishuhudia