Meneja
Mkuu wa Benki ya Exim tawi la Arusha Bw. Fredrick Umiro (kulia)
akikabidhi vyandarua vyenye dawa kwa Mtaalamu wa masuala ya upasuaji
katika hospitali ya Mount Meru iliyopo jijini Arusha, Dkt. Zubera
Mtengwa (wa pili kushoto).Wakishuhudia pembeni ni Meneja Mauzo wa benki
ya Exim Arusha Bw Bw. Assed Ali Naqvi (kushoto)na wawakilishi kutoka
hospitali hiyo.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Malaria
Duniani inayoadhimishwa kote ulimwenguni Aprili 25 ya kila mwaka
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Ligula iliyopo Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Gwao (wa
pili kulia) pamoja na Meneja Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Benki
ya Exim Tawi la Mtwara Bw. Chande S. Chande (kulia) wakionyesha baadhi
ya vyandarua vilivyowekewa dawa ikiwa ni msaada kutoka benki hiyo.
Wakishuhudia tukio hilo ni baadhi ya wawakilishi kutoka benki ya Exim
Mtwara na hospiatali hiyo. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku
ya Malaria Duniani inayoadhimishwa kote ulimwenguni Aprili 25 ya kila
mwaka.