https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    WAKANDARASI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA KAZI ZAO

    picha maktaba 

    Na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog.
     
    Wakandarasi nchini wametakiwa   kuzingatia ubora ,viwango  vya kazi zao ili kuweza kutekeleza kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuweza kufanya bkazi yenye viwango vya hali ya juu pindi wanapo tekeleza miradi mbalimbali nchini.


    Endapo wakandarasi wazawa wataweza kuzingatia taratibu za viwango vya ujenzi  pindio wanapopata zabuni za miradi ya ujenzi hali hiyo itaongeza chachu ya mabadiliko na kuweza kushasishi serikali kuyweza kuwa wanawatumia wakandarasi wazawa ili kuepuka gharama za kutoa zabuni kwa wakandarasi wageni  ili kuweza kutumia ghara ma ndogo na pesa  ziweze kubaki nchini na kutopelekwa kwa nchi za wakandarasi wageni.




    Hayo yameelezwa leo na Mhandisi   Omari Kiure  kutoka kampuni ya Kiure Engineering Limited kutoka mkoani hapa  wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi  jengo la kituo cha jimolojia  Tanzania  ambapio kituo hicho kiko chini  ya Wizara ya nishati na madini ambacho kimejengwa eneo la njiro mkoani Arusha. 


    Hata hivyo jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ambalo nikituo cha kutoa mafunzo kwa wanafunzi namna ya kuongeza thamani madini ya vito,mafunzo ya ukataji  madini ,utengenmezaji   bizaa za mapambo  sambamba na uchongaji vinyago vya mawe ili kuweza kuongeza ajira kwa vijana walio wengi ambalo ndilo kundi kubwa nchini ambalo halina ajira.


    Aidha aliongeza kuwa  endapo wkandarasi watajizatiti  na kuboresha kazi zao wataweza  kufanya kazi  ambazo zinzonekana katika viwango vya hali ya juu ili kuwezaa kushawishi wadau mbalimbali kuweza kuwapa miradi ya ujenzi pindi inapohitajika na kuweza kutokuwepo dosari ama kuanguka kwa magorofa baada ya muda mchache hali inayogharimu Serikali fedha nyingi ambazo bni kodi za wananchi.


    Kwa upande wake mhitimu wea kituo hicho Bi,Salome Mollel  alisema kuwa  ujenzi wa kituo hicho kitakuwa mkombazi wa vijana kupata mafunzo hayo na kuweza kupata ajira kwa wafanyabiashara wa mawe  kwani kulikuwa na changamoto kubwa sana ya kituo cha mafunzo ya uongezaji thamani ya vito vya madini hali iliyokuwa inawalazimu wafanyabiahsra hao kuuza madini yakiwa ghafi nsa kuuza kwa bei ya hasara  na fedha nyingi kuenda nchi nyingine.

    Ambapo kupitia kituo hicho kitawasaidia vijana kupata ajira na kuongeza thamani ya madini hayo na itawawezewsha wafanyabiahsra hao kuuza madini yakiwa yameongezwa thamani ili kupata bei nzuri na fedha kubaki na kuomgeza uchumi wan chi.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WAKANDARASI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA KAZI ZAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top