Hakuna
mtu anayejua kila kitu. Ni wazi hata sisi hatujui kila kitu. Pamoja na
hayo, tunapenda sana kujifunza. Tunajifunza kwa niaba yetu na kwa niaba
yako msomaji. Yale tunayojifunza tunajaribu kukushirikisha ili
tusaidiane. Tunajifunza kwa njia nyingi zikiwemo utafiti na majaribio.
Nia ni kuwa na uhakika kabla ya kukuletea tulichojifunza.
Zaidi ya hapo tunaongea na watu tofauti walio karibu na sisi au tunaoweza kuwasailiana nao kwa njia moja au nyingine ili kupata uhakika na kupanua mawazo. Unapojifunza kwa kutumia pia mawazo ya watu wengine (hata kama yanatofautiana na ya kwako) unajifunza zaidi.
Leo tumeona tuongelee kuhusu hii kitu inaitwa colour blocking katika fashion (Jinsi ya kuvaa nguo za rangi zilizo kali au zinazong’ara (Bold colors) na zaidi jinsi ya kuzipangilia hizo rangi ili upendeze.
Najua hata wewe umesikia watu wakisema “colour blocking outfits“. (Kama hujawahi sikia, leo nakupa fursa ya kuzijua na kujifunza) Fashionista/Celebrities hata models kwenye fashion shows unawaona wamevaa hizi kiaina fulani. Ukiwaangalia wanapendeza sana. Wakati mwingine ukitembea barabarani unakutana na watu (wale watiririkaji wa mwendokasi) wakiwa wamejivalia tu halafu ukimuangalia unaona mhmh (inabidi ujinyamazie tu, ndio kashaamua kuwa kwenye trend)
Lakini unakuwa huelewi kwamba inakuwaje unaona wengine wamependeza na wengine hawajapendeza? Ni vigezo gani hivyo wanatumia kujua kuzipangilia? Unatamani na wewe uvae lakini sasa kila ukijaribu unakuta mambo hayaendi kabisa. Ndio kwanza unaonekana kichekesho. Mwisho wa siku unajiamulia, aah wacha tu nikajivalie nguo zangu nyeusi.
Najua wengi tumehangaika au bado tunaangaika na hii issue ya jinsi ya kupangilia hizi rangi ili tusionekane kichekesho. Katika research zangu hii pia ilikuwa moja ya vitu vilivyonichukulia muda kujifunza. Na wala nisikudanganye bado najifunza kila muda unavyoenda.
Nimejifunza mengi kuhusu hizi rangi, kuanzia jinsi ya kuzipangilia kama vazi mpaka jinsi ya kupamba nyumba yako. Nimejifunza hata jinsi ya kumsoma mtu tabia kutokana na hizi hizi rangi na mengine mengi. Na bado naendelea kujifunza. Lakini leo nimeona niwaonjeshe kidogo niliyojifunza katika fashion sense.
Kitu cha kwanza kabisa ambacho niliona ni muhimu sana kuzingatia, ni kuzijua kiundani hizi rangi. Ni rangi gani hizo zinazojulikana kama color blocking? Je nawezaje kuzipangilia katika mavazi ili nisionekane kichekesho? Na je ni sehemu gani naweza kuzivaa bila kuwa judged? Ikabidi nianze research. Nikagundua vifuatavyo katika kupangilia nguo. Fuatana na mimi kujibu maswali yangu ya hapo juu.
Kwanza kabisa ni umuhimu sana kuzijua rangi zinazozungumziwa. Hapo juu ni mzunguko wa hizo rangi 12. Wenyewe wanaziita hue colors au color blocking. Sote tunajua ili kutengeneza kitu kizuri kinachopendeza lazima utumie rangi kuking’arisha.
Lakini kabla hakijan’gaa lazima ujue jinsi ya kuzipangilia rangi hizo katika muonekano uutakao. Basi hivyo ndivyo wajuzi walipoona watengeneze huu mzunguko ili watu kama sisi tujue jinsi ya kuzipangilia rangi hizi na kutupendezesha badala ya kujichangaya na kuchekesha.
Na kimojawapo cha vitu muhimu kujifunza katika mpangilio wako wa rangi, ni kwenye mavazi. Unaweza sema pia decorations za nyumba, na vingine vingi kwani sio kila mtu hivi hivi tu anajua kama orange na blue ni rangi zinazoendana vizuri bila kuujua vizuri huu mzunguko.
Kwahiyo ndio maana nasisitiza sana kwako kuujua huu mzunguko kwanza, kabla hujaanza kuvaa color blocking outifits. Kuzijua hizi rangi kiundani zitaweza kukusaidia kuchagua ni rangi gani zinazoendana katika mavazi, katika kupaka rangi nyumba, au katika kupamba kama wewe ni mpambaji. Na pili ni muhimu sana kujua ni rangi gani kati ya hizi zinaendana na ngozi yako ya mwili (skin tone), ili uweze kuzipangilia vizuri kwa muonekano wako binafsi katika mavazi.
Katika hii chart, kuna rangi 12, najua utakuwa unajiuliza sasa hii inakusaidiaje katika kuvaa? (Mavazi)
Kutokana na hiyo chart kuna njia rahisi ya kujua rangi gani zinaendana na rangi gani na jinsi ya wewe kuelewa namna ya kuzipangilia. Wamezigawa katika hivyo vifungu 9 tofauti na wakavitenganisha kwa majina.
Moja wapo ni Primary; hizi ni rangi tatu zilizoanzisha mtiririko wa rangi zote hizo 12. Rangi hizo ni Njano, nyekundu na blue).
Nyingine ni Analogous
Hizi nazo ni rangi zinazofuatana kutoka katika mchanganyiko wa rangi za primary. Mfano njano, orange na red, au Red violet, violet na blue violet.
Kundi lingine ni Complimentary
Hizi ni rangi zinazoangaliana kutoka upande tofauti (opposite ends.). Mfano wa rangi hizo njano na violet , au nyekundu na kijani, au hata Blue na orange.(kutokana na mduara wa hizi rangi hapo juu)
Tukianza angalia (Primary colors) ni muhimu sana kujua kwamba hizi rangi tatu(Njano, Nyekundu na Blue) ndio mwanzo wa hizo rangi zote 12. Rangi hizo zikichanganywa moja baada ya nyingine ndio rangi hizo nyigine zinapatikana.
Kwa mfano rangi ya Njano na nyekundu, zikichanganywa inapatikana rangi ya orange, au Njano-orange, na pia inapatika nyekundu- orange. Kufahamu huu mchanganyiko ni mwanzo wa kujua rangi gani na rangi gani ukizivaa zinaweza kuendana, au kupendeza kwasababu ni rangi zilizoingiliana. Kwa mfano hapo; unaweza kujua kumbe unaweza changanya rangi ya njano, nyekundu na orange katika vazi lako na ukatoa muonekano mzuri kwasababu zinaingialiana.
Ukifatilia zaidi utajua kumbe hata rangi kama blue na njano, mchanganyiko wake unapata kijani. Ndio maana ukivaa rangi ya njano na kijani vinaendana, kumbe kijani imetoka kwenye njano na blue, information hii imenisaidia sana mimi kujibu vimaswali vyangu vilivyokuwa vinanisumbua.(Kwanini wengine wanapendeza na wenginw siwaelewi elewi)
Zaidi ya hapo, mimi ni mpenzi mzuri sana wa rangi ya violet (mimi nimezoea kuiita Lilac, au wengine wanaijua kama light purple) katika hili nimejifunza sana kwasababu rangi nyingine niipendayo ni nyekundu na blue, lakini nilikuwa sijui sana jinsi ya kuzipangilia rangi nizipendazo, kujua kwamba lilac (vilot) imetoka katika hizo mbili,(Red na blue) imenisaidia kujua jinsi ya kuzipangilia nguo zangu zaidi, hasa nikiamua na mimi kutiririka na color blocking.
Chini ni mpangilio tu wa colour blocking kwa ujumla.
kuweza pata huu muonekano unaweza bonyenza links hapo chini.
1.handbag
2. Shoes
3. Skirt.
4.Blouse
5. Belt
Analogous colors ; Hizi ni rangi zozote tatu katika hiyo chart ambazo zinafuatana, na zilizokuwa karibu na nyingine. Kwa mfano njano, njano-orange na orange, au Red, red-violet na violet, n.k. Hizi pia ni rangi ambazo unaweza kuzichanganya katika mavazi yako na ukapendeza. Lakini katika hizi rangi jaribu sana kuepuka kutumia “hue colours” katika muonekano mzima.
Hapa sasa, hue colors kama nilivyosema mwanzo ni hizo rangi zote 12 unazoziona hapo katika chart. Hizi rangi kwa maelezo ya wataalamu, ni zile zilizokuwa sharp, yaani ni kali katika muonekano kwasababu ni kali sana machoni mwa watu ukizivaa, wakaona haipendezeshi sana au haioneshi muonekano mzuri kama wanavyotaka.
Wakaamua kuzigawa kwenye makundi mawili. Kundi la kwanza zikachanganywa na rangi nyeupe, wakaziita Tint colors na group ya pili zikachanganywa na rangi nyeusi wakaziita Shade colors.
Kutaka kuzijua vizuri angalia hiyo chart hapo juu. Na hata ukiwa unanunua nguo za rangi hizo, utaona kabisa kuna nyingine zimekolea sana rangi na nyingine zinaelekea weupe na nyingine zimedidimia rangi kidogo kuelekea weusi.
Hapo ndio ninaporudia pale niliposema kwamba katika muonekano wako wa siku katika outfit yako jaribu kutovaa hizo rangi za hue. Badala yake wanashauri zaidi jaribu kuchanganya na rangi wanazoziita “Tint analogiuous colors”. Mfano labda umevaa shati la hue blue, basi labda sketi iwe ni aina ya rangi ya Tint green(Kijani) badala ya hue green (kijani)
Na hii ni mifano ya nguo za analogous zinavyoendana.
Complementary colours; Hizi ni rangi mbili zozote zinazotofautiana katika hiyo chart, ambazo zinaangaliana kutoka upande tofauti. (Opposite end) kutokana na huo mchoro hapo juu wa rangi; Kwa mfano; Blue na Orange(zinvyoangalina) au Nyekundu na Kijani.
Kwa Mujibu wa wataalamu, hizi rangi zikivaliwa pamoja zinaendana vizuri sana na zinapendezesha muonekano mzima. Ni rangi tofauti kabisa, kwa maana haziingiliani kabisa kama rangi za analogious.
Kwa kuwa ni rangi zisizoingiliana kabisa wanasema ni rangi ambazo rahisi sana kuanza nazo, kama wewe ndio kwanza unajifunza jinsi ya kupangilia hizi color blocking outfits. Ushauri mkubwa ambao nimeuona kila mahali na wanasisitiza sana , ni kuwa wakati unazivaa rangi hizi (complementary colors) tumia rangi moja wapo kama background(inayobeba muonekano) kwa mfano Gauni zima na nyengine kama accents(inayorembesha muonekano) kama handbag, viatu au belt.
Na kama unavaa chini na juu, waweza tumia rangi za tint,(zile zilizochanganywa na rangi nyeupe) ukachanganya na rangi za “Shade”( zile zilizochanganywa na rangi nyeusi) katika kutofautisha juu na chini. Mfano unaweza vaa light (tint blue) na dark (shade orange) au pia unaweza vaa suruali ya hue blue ukavaa na blouse rangi ya tint njano.
Mfano wa nguo zilizofuata complementary colors
Aina hizi za nguo za complimentary color zinaonyesha utofauti mkubwa sana kwenye rangi na katika muonekano, lakini ni mchanyanyiko mmoja ambao unapendezesha sana. Muhimu sana kuwa mwangalifu unavaa wakati gani, kwani ni muoneknao unaoweza kuonekana kwa distance ya mbali sana; wanaziita ( pure bold colors) hakikisha unavaa pale tu unapotaka ku stand out kwenye kadamnasi.
Hapa hapa kwenye complimetary colors, kuna kitu kinaitwa Split complimentary colors; Hii ni jinsi tu ya kutumia rangi tatu katika muonekano mmoja. Unachukua rangi moja kutoka kwenye hue colors, una match na rangi nyingine mbili, kama rangi ya blue ukachanganya na rangi ya njano-orange (yellow-orange) au na nyekundu- orange (Red- orange). Hii ni muhimu sana kujua ni rangi gani zinaingiliana ili uweze kuzipatia vizuri.
Chini ni mifano ya Split complimentary colors.
Tip ya mwisho ambayo nimeona ni muhimu sana kuweka hapa ni kutofautisha kati ya hizi rangi zaidi. Kuna aina nyingine mbili, rangi za warm(joto) na rangi za cool (baridi). Kwa undani zaidi hizi ni rangi ambazo wametofautisha kwa kuzigawa tena kwenye mafungu mawili kutofautisha zipi zaweza valiwa wapi na zipi zinaelezea tabia ya mtu tukiongelea kwenye mavazi.
Aina hizi mbili zinavaliwa sehemu tofauti, kwa mfano Cool colors, hizi ni zile rangi zinazotakiwa kuvaliwa zaidi makazini, sehemu za heshima, kwasababu ni rangi zinazojulikana kuwa na sifa(characteristics) za kuwa Cool, kwamba zimetulia, calm na ziko ki proffesionals zaidi. (sasa kama wewe ni wale wa bold characters (wale wanaopenda kujilipua na kutiririka) basi wakati wa interview au nguo za kazini jaribu kukaa upande wa kulia kwenye rangi za cool.
Warm colors ni zile bold, zile zinazowaka kutoka mbali, kali, na zipo upande wa kushoto.(katika picha ya hapo juu), hizi wanasema zina sifa ya kuonyesha furaha, mcheshi na mtu anae take risk, na mengine mengi; hizi wanashauri unaweza vaa wakati wa furaha (have fun) kama club, lunch na marafiki zako sehemu ambayo sio sehemu za mambo ya serious.
Kitu kingine nilichojifunza katika hizi rangi za cool and warm colour ni jinsi zinavyoweza kumuelezea tabia ya mtu kwa jinsi tu ya anavyochagua na kuzitumia hizi rangi (kumjua ni mtu wa aina gani) Well hiyo nayo ni topic nyingine mpya kabisa.
Baada ya information na mifano yote hapo juu, nahisi kidogo utakuwa na idea ya jinsi ya kuanza, usisite kuendelea kufanya zaidi research kujua kiundani zaidi. Huu ni mwanzo tu.
Kuogeza kidogo unaweza anza na hizo rangi za hapo juu, kutengeneza rangi zako za “color blocking” Fatilia jinsi walivyoambatanisha rangi za kuchanganya.
Zaidi ya hayo, matarajio yangu tumesaidiana kidogo pa kuanzia. Ninachoweza kusisitiza tafadhali sana tengeneza rangi zako mwenyewe zinazokupendeza wewe kama wewe. Sio kila rangi inaweza mpendezesha kila mtu.
Hakikisha unafanya majaribio ili uwe na uhakika na muonekano wako wewe mwenyewe. Confidence is the key. Na pili usisite kutuandikia au kutushauri pindi utakapoweza kugundua mengine katika topic hii, ili nasi tujifunze zaidi, au kama una swali lolote ambalo tunaweza kusaidia kuelekezana zaidi.
Till next time, Stay safe.

0 comments:
Post a Comment