Tuliziona
pichaz Yamoto Band pamoja na story za wao kwenda zao London, Uingereza
kupiga show, siku ya leo FEB21 muda mfupi baadaye watakuwa na show, watu
wetu hawa saa chache zilizopita walikuwa kwenye Interview na mtangazaji
Charles Hillary kwenye BBC Dira ya Dunia.
Swali la
kwanza kuulizwa ilikuwa wapi lilikozaliwa jina la Yamoto Band?
;”Ukiachana na vitu vya motomoto ambavyo tunavitoa ni jina ambalo
lilibeba nyimbo yetu ya kwanza.. Yamoto Band ni zao la Mkubwa na Wanae,
kituo ambacho kinalea watoto wenye vipaji..“– Aslay.
Kuhusu
ishu ya mtu anayewaandikia nyimbo zao; “Mara nyingi sana tunaandika
wenyewe lakini tunashare idea na bosi wetu Mkubwa Fella.. Tunakaa naye
na tunashare idea“– Aslay.
Hapa
wanaongelea utofauti wa Yamoto Band na band nyingine; “Vitu vingi
vishafanyika, uongozi wetu unataka sisi tuwe wapya ndio maana bendi
unaona iko tofauti kwanza tuna umri mdogo.. nyimbo zetu zina dakika tatu
nne tofauti na bendi nyingine..“– Maromboso.
Band
nyingi zinavunjika, unadhani hii itatokea kwa Yamoto?; “Sisi tumekaa ni
zaidi ya miaka minne tuko pamoja kabla ya Yamoto Band kujulikana tunajua
nini maisha halafu tumetoka katika maisha magumu.. Sio rahisi leo
unishawishi kwa vitu vidogo milioni mbili milioni tatu wakati
tunategemea mamilioni mengi baadaye“– Aslay.
Ni nini
siri ya umoja wao?; “Tumekaa muda mrefu sana kwenye tundu moja kwa hiyo
tumeshazoeana hata tabia zetu.. Tumeshakuwa kama ni ndugu sasa na sio
marafiki tena“– Bella.
Hapa
Charles aliomba kuambiwa maana ya ‘Kupwelepweta‘; “Kupwelepweta ni kitu
ambacho hakikutoshi, kama mimi nivae koti lako lazima linipwelepete…“–
Aslay.
Hii ni sauti ya Interview yao yote nimerekodi BBC Dira ya Dunia, play kuisikiliz