Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IMEKULA
kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa
muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye
misiba ya wenzake.Wakizungumza
na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes
‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba
majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha
kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo
itampa ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.
“Mimi
nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa
sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha
kwenye media.
“Halafu
akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile
alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya
hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii
mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa
tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini
ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake.”

