Na BIN ZUBERY
BEKI wa
Mbeya City, Juma Said Nyosso amefungiwa mechi nane kwa kosa la kumtomasa
sehemu za siri mshambuliaji wa Simba SC, Elius Maguri timu hizo
zilipokutana Januari 28, mwaka huu.
Habari
kutoka ndani ya kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) jana zimesema kwamba, mbali na Nyosso, beki wa Azam FC,
Aggrey Morris naye amefungiwa mechi tatu.Juma Nyosso kuli amefungiwa
mechi nane kwa kosa la kumdhalilisha Elias Maguri
Morris
amefungiwa mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kwa makusudi
kisukusuku mshambuliaji wa SImba SC, Emmnauel Okwi timu hizo
zilipokutana Januari 25, mwaka huu
Okwi
alipoteza fahamu baada ya kupigwa na Aggrey na kulazimika kukimbizwa
hospitali ya Rufaa ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi
na taarifa za Madaktari zilisema Mganda huyo angeweza kupoteza uhai
siku hiyo kama si kuwahiwa kwa huduma ya kwanza.
Mechi
zote hizo zilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC ikitoa
sare ya 1-1 na Azam FC kabla ya kufungwa 2-1 na Mbeya City.
Katika
kikao chake cha awali, Februari 3, mwaka huu Kamati hiyo ya Nidhamu
ilitoa adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja
kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kinidhamu.
Kamati
hiyo iliwafungia mwaka mmoja viongozi wawili wa Chama cha Soka Wanawake
Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza kwa kuwashawishi wachezaji wa Mwanza
Queens kugomea uamuzi halali.
Sophia
Tigalyoma (Mwenyekiti) na Katibu wake Hawa Bajanguo walitiwa hatiani kwa
kuwashawishi wachezaji kugomea uamuzi wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa
Wanawake ya TFF kutupa rufani yao dhidi ya Kigoma.
Kocha wa
Polisi Tabora, Eliakim Christopher amefungiwa mechi kumi na kupigwa
faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 39(2) ya Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) baada ya kutiwa hatiani kwa kumtukana refa wakati wa mechi
kati ya timu yake na Panone FC iliyochezwa mjini Moshi.
Aggrey Morris kulia amefungiwa mechi tatu kwa 'kutaka kumuua' Okwi
Wachezaji
wa JKT Oljoro FC, Dihe Makonga, Swaleh Idd Hussein, Ramadhan Mnyambegu
na nahodha Shaibu Nayopa wamefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 300,000
kila mmoja kwa kuzingatia kanuni ya 36(10) ya FDL kutokana na kufanya
vurugu kwenye mechi kati yao na Burkina Faso iliyochezwa mjini Morogoro.
Mtunza
Vifaa (Kit Man) wa JKT Oljoro FC, Eliud Mjarifu amefungiwa miezi sita na
kupigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumpiga Kocha wa Burkina Faso, CR
Mwakambaya kwenye mechi kati ya timu hizo iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro.
Pia
Mjarifu amepewa onyo kali na kutakiwa kutorudia tena kutenda kosa, kwani
hata mwenendo wake wakati wa shauri hilo ulionyesha utovu wa nidhamu
mbele ya Kamati.
Naye
Mtunza Vifaa wa Rhino Rangers FC, Albert Mbuji amefungiwa miezi sita na
faini ya sh. 200,000 kwa kupatikana na hatia ya kuwatukana na kugomea
uamuzi wa marefa kwenye mechi dhidi ya Polisi Dodoma. Adhabu hizo
zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya FDL.
Kamati
hiyo imeondoa malalamiko dhidi ya Ofisa Habari wa klabu ya Ruvu
Shooting, Masau Bwire kwa vile refa Israel Mujuni Nkongo ambaye ni
mlalamikaji hakufika kwenye shauri hilo.
Nkongo
alimlalamikia Bwire akidai alitoa maneno yenye kuweza kuchochea chuki
dhidi yake kwa waamuzi, kwani kupitia redio 100.5 Times FM, Bwire alidai
refa huyo ndiye aliyeshinikiza kuondolewa kwa refa Mohamed Theofil
kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Pia
Kamati hiyo imemkuta bila hatia Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda ambaye TFF ilimlalamikia
kuwa akiwa mtendaji mkuu wa chama hicho alishindwa kuhakikisha timu ya
Singida inaingia uwanjani kucheza na Dodoma kwenye mechi ya Kombe la
Taifa kwa Wanawake.
Kamati
ilikubaliana na utetezi wa Gunda kuwa, jukumu la timu hiyo lilikuwa
mikononi mwa viongozi wa TWFA Singida, na tayari SIREFA kupitia Kamati
yake ya Nidhamu ilishatoa adhabu kwa viongozi wa timu hiyo kutokana na
kitendo hicho.
Nayo
malalamiko ya Polisi Tabora FC kutaka mechi yao dhidi ya Toto Africans
FC irudiwe kwenye uwanja huru (neutral ground) kwa madai ya kuchezeshwa
zaidi ya muda unaotakiwa, na kutokuwepo ulinzi wa kutosha kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekataliwa.
Pia
Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu za Mwadui FC na Polisi
Mara FC dhidi ya Toto Africans kwa kumchezesha mchezaji Ladislaus Mbogo
bila kuonyesha leseni yake yasikilizwe haraka na Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB) kwa vile si ya kinidhamu.



