Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta
katika kata ya Chalinze wakitokea jijini Dar es Salaam jana, kukagua
uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na
kuharibu makazi ya watu na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika
vijiji vya Msoga na Tonga
Na Freddy Maro Chalinze,Bagamoyo.
Jumamosi 21,February, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana
aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa
vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko
Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye
alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi
Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo
ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji
walioangukiwa na nyumba zao.
“Nimepata taarifa ya maafa
yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale
ambao nyumba zimeharibika serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi
akipata taarifa atajua jinsi gani ya kuwasaidia.Lakini kuna misaada
tunayoweza kutoa.Nasikia Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja
na matibabu.Lakini Kwenye serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo
taarifa zipilekwe kwake kwa uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana
tutaendelea kusaidiana,” alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa
kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.
Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo
mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya
Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti
kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika
hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika
na mkasa huo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi
wa kata Ya Chalinze wakikagua baadhi ya nyumba zilzoharibiwa vibaya
baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo
mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.Rais
Kikwete alikagua uharibifu huo, kuzungumza na kuwafariji wana vijiji hao
na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo

na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo(picha na Freddy