Waziri
Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa akiingia
katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki
ghafla jana.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.
Mwili wa Marehemu Salmin Awadh ukiingizwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.
Viongozi
mbali mbali wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa
heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa
Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akiongoza waumini katika Sala ya
Marehemu Salmin Awadh Salmin katika Masjid Noor Muhammad (SAW) uliopo
Mtaa wa Kwamchina mwanzo.
Viongozi
mbali mbali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt Ali Muhammed Shein wakimuonbea dua Marehemu Salmin Awadh
baada ya sala iliyofanyika Masjid Noor Muhammad (SAW).
Viongozi walioshiriki sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiagana baada ya kumalizika sala hiyo.
Naibu
Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Mwakilishi wa Jimbo
la Kikwajuni Mahmoud Muhammed wakibadilisha mawazo kuhusu msiba huo.
Mamia ya
wananchi waliohudhuria sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin
wakiutoa msikitini mwili wa marehemu kuelekea kijijini kwao Makunduchi
kwa mazishi.
Msafara
uliobeba mwili wa Marehemu Salmin ukiondoka Masjid Noor Muhammad (SAW)
kuelekea Makunduchi kwa ajili ya mazishi. (Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar).