WANANCHI WAKIMSIKILIZA MKUU WA POLISI TUKUYU MWENYE KOTI JEUSI KULIA AMBAYE NAYE AMEWATAKA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUKIMBILIA MATUKIO YA AJALI |
MMOJA WA WAGOJWA WALIO KATIKA HALI MBAYA KATIKA HOSPITAL YA IGOGWE WAKIENDELEA NA MATIBABU |
MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO AKIUGULIA VIDONDA NA MAUMIVU YA MOTO |
Watu watatu wamefariki dunia kwa ajari ya moto akiwemo
utingo wa gari hilo aliyefia hospitari kwa kuvuja damu nyingi na watu kumi na
nne kujeruhiwa na kulazwa katika hospitari ya Igogwe na watutu kuthibitishwa na
Dactari kuwa hali zao ni mbaya baaada ya gari aina ya scania lenye namba za
usajiri T821ARF mali ya kampuni ya Irasi likiwa limebeba mafuta ya petrol,
kuacha njia na kupinduka mida ya saa
tatu usiku eneo la kijiji cha Isongole (namber one )kata ya Isionje .
Moto huo uliosababishwa na mwanamke aliekuwa na kibatari
kwenda kumulika mafuta katika mfereji wa maji uliopo eneo la tukio
kwa kibatari chake ili ajue kama yale ni
mafuta au maji kitendo kilichosababisa
moto kuwaka kufuata mafuta yaliyo kuwa yakimwagika mpaka eneo gari lilipoanguka
hivyo kusababisha watu mifugo na mashamba kushika moto.
Moja wa shuhuda wa tukio aliyejitambulisha kwa jina moja la Matola amesema kwamba gari lilianguka
mida ya saa tatu usiku ndipo wananchi walikimbilia kuchota mafuta na dereva na baabhi ya wakazi aliwaktaza
kusogea eneo hilo na kuwataka wawasaidie kutoka eneo hilo na baada ya
mda kidogo wao kutolewa ndipo moto
ulilipuka kutoka katika mfereji wa maji
na kusambaa kufuata mafuta yalipo hadi kufika kwenye gari.
Bwana Matola
alifafanua kuwa“ Tunashukuru moto uliwahi kuwaka kabla ya watu kujaa hata hivyo
baadhi ya wenyeji wa eneo hilo
walijitahidi kuzuia watu wasichote mafuta lakini wengine hawakuweza
kuwasikiliza wakizani kwamba watapata mafuta kama ilivokuwa juzi (siku tatu
nyuma )baadaya gari la mafuta ya dizeli kuanguka na wao kuchota mafuta mengi na
kuuza lita ishirini kwa shilingi elfusaba tu, hadi alipotokea mama moja ambae
ni moja wa waliofariki kuja na kibatari kumulika mferejini ili kujua kama yale
ni mafuta au maji na ndipo mafuta yakashika moto.”
Dereva wa gari hilo Zawadi nyato aliyekimbizwa hospitali ya
igogwe baada ya kupata ajari amesema kuwa alipokuwa kwenye mlima anashuka taa
ya upepo iliwaka kuashiria hakuna upepo na kwa sababu alikuwa amebeba mzigo mzito
gari likamshinda na kujikuta yuko hospitalibila kujua kilichoendelea hapo.
Nae mkuu wa wilaya Mhe. Chrispin meela amefika eneo la tukio
kutoa pole na lambi rambi kwa wakazi wa eneo hilo na kuwakumbusha kuwa wawe makini na vitu vya hatari kama hivi kwani
tukio kama hili liliwahi kutokea katika mtaa huo huo na kusababisah vifo vya
watu wengi lakini bado wanarudia kitendo kama hicho. Hivyo amewataka watu
wabadilike na wajifunze kupitia matukio yaliyopita.
Ajari ya moto kama hii iliwahi kutokea miaka ya 1990s katika
kata hiyohiyo ya Isionje mtaa wa numba one mita chache kutoka ilipotokea ajali hii ya leo na kuuwa
watu wengi waliozikwa kwa pamoja katika eneo hilo kwani walishindwa kutambulika
na ndugu zao na kijeruhi mamia ya watu.