Mhe. Stephen Wasira akichukuliwa vipimo na mbunifu wa mavazi, Sheria Ngowi.
BAADA ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutofunga vizuri vifungo vya suti yake,
Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona
mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea
suti zake.
Waziri Wasira akijaribu kurekebisha suti yake iliyokosewa kufungwa vifungo na kuzua mjadala mitandaoni.
Mhe.
Wasira ameamua kukutana na mbunifu huyo aliyeanza mara moja kumchukua
vipimo vyake ili amtengenezee mavazi yake ambayo atakuwa akiyatumia
katika shughuli zake mbalimbali za kiserikali.
Picha
za Waziri Wasira zilienea mitandaoni alipopiga picha ya pamoja akiwa na
Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la
suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.
Baadhi ya picha na katuni kutoka mitandaoni baada ya Mhe. Wasira kukosea kuvaa suti yake.
Baadhi
ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walirusha picha mbalimbali
zikimuonesha Mhe. Wasira huku mmoja wa watangazaji akisema kuwa iwapo
akikubaliwa, atajitolea kuwa wabunifu wa suti zake za mitoko ili jambo
hilo lisijitokeze tena.
Mhe.
Wasiara akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kanisa la Kisabato
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa
kufungwa vifungo.
Kwa
kuamua kumuona Sheria Ngowi, Mhe. Wasira atakuwa amepata mti shamba wa
tatizo hilo lililotawala mitandao ya kijamii hivi karibuni.

