
Mchezaji
wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa
timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la
Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es
salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0 zilizotiwa kimiani na Mshambuliaji
Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na 55. PICHA ZOTE NA OTHMAN
MICHUZI

Golikipa
wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana akiondosha hatari iliyokuwa
ikielekezwa langoni mwake wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani
Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga
imeshinda bao 2 - 0.

Winga
machachari wa Yanga,Saimon Msuva akiangalia namna ya kumtoka beki wa
timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana,Othusitse Mpharitlhe wakati wa
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa
Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.











