https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    ANGALIA PICHA ZAIDI YA 30 - TUKIO LA MVUA YA MAWE MAKUBWA KAMA NDOO ILIYOUA WATU WENGI HUKO MWAKATA-KAHAMA-SHINYANGA

    Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Mawe hayo ya mvua yanadaiwa kuwa na ukubwa wa ndoo ya lita 10,na yalikuwa yamezagaa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika.Pichani ni barafu ikiwa imeanza kuyeyuka


     
    Watu 38  wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
    Mbuzi wakiwa wamekufa
     Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada. 
     
     eneo la tukio

    Viongozi wakiwa eneo la tukio
      Nyumba ikiwa imeharibika vibaya,ambapo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyefika eneo la tukio 
     
     makazi hakuna Barafu maarufu MAWE ikiwa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika
     
     Hali halisi katika eneo la tukio
     Blog hii  imefika katika eneo la tukio na kushuhudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo.

    Moja ya nyumba zilizoharibika
     
     Kijijini Mwakata

    majaruba yakiwa yamefurika maji
     
     madhara ya mvua hiyo
     
     Madhara ya mvua


     Mazao shambani

     Miti imevunjika Eneo la Mwakata
      Jinsi Mimea ilivyoharibika
      Hali halisi eneo la tukio
     
    Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(pichani) amesema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
     
    Wananchi wakihangaika Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine  wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.



    Mpesya amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.


    Akiwa eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo. 

    Mwananchi akiwa haamini kilichotokea
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ANGALIA PICHA ZAIDI YA 30 - TUKIO LA MVUA YA MAWE MAKUBWA KAMA NDOO ILIYOUA WATU WENGI HUKO MWAKATA-KAHAMA-SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top