Dr.Twalibu Ngoma Proffesor na Mkuu wa Kituo cha Kliniki ya Mafunzo ya Sarataani kilichopo University ya Muhimbili Dar es salaam nchini Tanzania |
Mhe.Balozi Mulamula na waTanzania wanaDiaspora wakimpongeza Dr.Ngoma kwa furahaa
Uniting Africans in Diaspora (AID) Against Cancer;
Sehemu
ya pili ya kongamano la Global Health Catalyst cancer Summit
ilijumuisha wanaDiaspora waafrika ambao ni nguvu kubwa na rasilimali
endelevu kwa katika nchi zao za kuzaliwa. Ripoti ya utafiti uliofanywa
kwa baadhi ya viongozi wa USA Afrikan Diaspora imedhihirisha kuwa
karibu asilimia 90 % ya wanadiaspora wana nia na malengo ya kuleta
mabadiliko katika nyanja mbali mbali nchini mwao ukiwemo uwanja wa afya
barani afrika.
Dr. Doyin Oluwole
Mkurugenzi wa Taasisi ya Pink Ribbon Red Ribbon, jitihada zilizoanzishwa na Rais Mstaafu
Mhe. George W. Bush
|
Mashirika mbalimbali yalionyesha mipango ya ujenzi wa vituo vya kutoa tiba ya saratani nchin Tanzania
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Mhe. Iddi Sandaly alieleza nia ya wanaDaspora kuwa mstari wa mbele katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania na malengo ya kupeleka huduma ya afya kwa jamii zenye uhitaji hivi karibuni.
Mabigwa wa Saaratani mbalimbali duniani wakijadili njia bora za kuborehsa huduma za saratani.
Ukosefu
wa Elimu Afya kwa jamii ni kati ya changamoto zinazopelekea ongezeko la
vifo vya gojwa la saratani barani Afrika. Saratani nyingi huweza
kutibika endapo zimegundulika mapema na kupata utafiti na huduma sahihi.
Mwanzilishi
wa http://www.nesiwangu.com/ ; mtandao unahusika na utoaji wa Elimu
Afya kwa lugha ya kiswahili Bi. harriet Shangarai, alizungumzia faida
za kutoa Elimu Afya kwa kutumia lugha ya asilia na kusema kuwa baadhi
ya wasomaji wake walitafuta huduma ya haraka baada kujisomea na kuelewa
dalili zenye kuashiria hitilafu katika mifumo mbali mbali mwilini. Bi.
Harriet alizungumzia faida zitokanazo na Teknolojia ya mawasiliano
ambayo ni fursa kubwa kwa Wanadiaspora kutoa mchango wao wa kielimu kwa
jamii na kujenga mawasilino ya karibu na wataalam wa afya nchini mwao
ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika kuziba mapengo yaliyomo
kwenye uwanja wa huduma na elimu ya afya.
Wataalam
wa afya katika diaspora walipata fursa ya kujadili njia mbali mbali
zitakazowawezesha kushirikiana na kupata fafanuzi za huduma za afya
nchini mwao.
Taasisi binafsi na vyombo mbali mbali vinavyotumika kuboresha huduma za saratani barani Afrika
Afrikan Women cancer Awareness association (AWCAA)
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa African Women Cancer Awearness association NGO ( AWCAA)
Mrs.Ify
Nwobuke (kushoto) na Mwakilishi wa AWCAA (kulia), walizungumzi huduma
za saratini ya matiti mbazo wamekuwa wakizitoa barani Afrika. Mrs Ify
alisema saratani ya matiti yaweza kutibika iwapo imegunduika mapema
hivyo elimu kwa jamii ni muhimu katika mapambano ya saratani.
Shukrani;
Waandalizi wa Global Health Catalyst Cancer Summit @ Harvard Medical School, 2015
Kwa maelezo zaidi pitia