Na. Anitha Jonas na Johary Kachwamba -MAELEZO, DODOMA
WAZIRI
wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka amesoma Muswada wa Sheria ya
Kuratibu Ajira za Wageni nchini wa mwaka 2014 kwa mara ya pili ikiwa
muswada huu umelenga masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi
pamoja na mahitaji ya kiteknolojia ambayo ni kichocheo kikubwa cha
uhamiaji wa nguvu kazi kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Mhe.Kabaka
alisema kwa sasa zipo mamlaka nyingi zinzotoa vibali vya ajira kwa
wageni kwa kuzingatia sheria zinazosimamia maswala ya Uhamiaji,
Uwekezaji, Elimu, Biashara na Wakimbizi, hivyo hali hii ya kuwepo na
mamlaka nyingi zinachangia kusababisha usumbufu kwa wawekezaji na
kokosekana kwa uwajibikaji pamoja na kuwepo na udanganyifu.
“Kutungwa
kwa sheria hii kunalenga kutelekeza kwa manufaa ya nchi yetu mikataba
ya kikanda inayoruhusu uhamiaji huru wa nguvu kazi hususani inayohusu
itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afika Mashariki na Ushirikiano
wa Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika SADC” alisema Mhe. Kabaka.
Katika
kutekeleza mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu uhamiaji na nguvu
kazi, utaratibu wa kutoa vibali vya ajira kwa wageni umekuwa ukitumika
ili kuhakikisha nguvu kazi ya wageni hao inaleta manufaa kwa maendeleo
ya kiuchumi na kijamii, na pia katika kulinda ajira za wananchi.
Kwa
upande wa Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Mhe.Celina Paresso
Mbuge wa Viti Maalum-CHADEMA aliishauri Wizara ya Kazi na Ajira
kushirikiana na wizara mtambuka kama Wizara ya Viwanda na Biashara na
Idara ya Uhamiaji, kufanya ukaguzi wa vibali vya ajira hasa katika
maeneo ambayo raia wa kigeni wanafanya shughuri zao bila kuzingatia
sheria za nchi.
“Tanzania
tuna maliasili nyingi, lakini dunia ya leo na ijayo itatawaliwa na
wenye maarifa, kwa maana ya sayansi, teknolojia, elimu na ujuzi” alisema
Mhe. Paresso
“kuwa
na maliasili peke yake haitoshi, hatuna budi tujinoe kwa elimu na ujuzi,
na hasa elimu inayomuwezesha mtu aajirike au ajiajiri” aliongezea Mhe.
Paresso
Endapo
Mhe. Rais ataridhia, Sheria hii itaanza kutumika tarehe 1 Julai, 2015.
Kutungwa na kuanza kutumika kwa Sheria ya Ajira ya Wageni Nchini
kutakuwa na matokea chanya ikiwema uratibu mzuri wa ajira za wageni
nchini, kuongezeka kwa ajira za watanzania na kuongezeka kwa ujuzi kwa
wafanyakazi wa Tanzania.

