Meneja
Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF.Bw. Aloyce Ntukamazina
akiwasilisha mada juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika Mfuko
wa GEPF,wakati wa semina kwa Maafisa Rasilimali Watu kutoka Wilaya ya
Ilala iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock,jijini Dar es salaam.
Meneja wa GEPF mkoa wa Ilala,Bw Jafari Meraji akisisitiza jambo juu ya faida zipatikanazo katika mpango wa hiari wa kujiwekea akiba (VSRS)
Mmoja
wa washiriki wa semina hiyo Bw Sebastian Enosh ambaye ni Meneja
Rasilimali watu kutoka DIT akitoa mchango wake pamoja na ushauri kwa
Mfuko wa GEPF.
Pichani baadhi ya washiriki wa semina hiyo maalum wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa GEPF.
Maafisa
Rasilimali watu wakipata maelekezo ya kujaza fomu na kujiunga na mpango
wa hiari wa kujiwekea akiba kutoka kwa Afisa Masoko wa GEPF Bw Avit
Nyambele.

