Kwa wale
wasiomfahamu sawasawa muuaji huyo, anaonekana mara kwa mara katika
runinga akiwachinja bila huruma watu waliotekwa na kundi lake la IS.
Wamarekani wanamsaka kila kukicha!
Sasa Mei
22, 2009, John akiwa na wenzake wawili walitua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa lengo la kuingia nchini ambapo
habari za ndani kutoka uwanjani hapo zinasema walikuwa wafikie Masaki
kwa mwenyeji wao mmoja ambaye ni raia wa Yemen.
Inadaiwa
kuwa, John na wenzake walikuwa wamekuja nchini kwa utekelezaji wa
mafunzo ya vitendo vya kigaidi nchini lakini azima yao hiyo ikaishia
mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Kikuu cha JNIA, Dar baada ya
kubainika kuwa, walikuwa wamelewa tangu wakiwa ndani ya ndege.
Hivi
karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe amesema kuwa, John
na marafiki zake hao walizuiwa kuingia nchini mwaka 2009 kwa sababu
walikuwa wamelewa sana na kuwatukana maafisa wa uhamiaji wa uwanja huo.
Alisema
John na wenzake walitua Dar saa 10 jioni wakiwa ndani ya ndege ya KLM
kutoka Amsterdam (Uholanzi). Waziri Chikawe alisema rubani wa ndege hiyo
ndiye aliyewataarifu maafisa wa uhamiaji hao kwamba kulikuwa na watu
kwenye ndege wamelewa kupindukia.
Habari
nyingine zilidai kuwa, John na wenzake walikuwa waungane na mwenyeji wao
kwa safari ya nchini Somalia ambako alitakiwa kwenda kuanza kuchinja
wanajeshi wanaoisaidia serikali ya nchi hiyo.
Hata
hivyo, habari nyingine zinadai kuwa, mwenyeji wao huyo alikimbia nchini
baada ya kuhisi kusakwa na maafisa usalama huku akienda kuwashitaki John
na wenzake kwa kulewa kupita kiasi huku wakijua walikuwa na kazi nzito
mbele yao.
Katika
kituo hicho cha polisi uwanja wa ndege, John na wenzake walilala kwa
siku moja kabla ya kurudishwa walikotoka huku baadhi ya maofisa
wakiambiwa na mahabusu kuwa, John na wenzake walikuwa wakizungumzia
mambo ya mauaji kwa muda mrefu