https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Juan Mata: Tumesikia, Tumeona, na Tumeamini Uongo Uliosisitizwa


    mataNa. Nicasius Coutinho Suso
    Miaka haisimami,  siku hazigandi na mshale wa saa hauna subira. Ndio hivyo unavyoweza kuyazungumzia maisha ya mwanadamu,  hatuna budi kuwa makini kuendana na kasi hii. Ni kama ambavyo hayati Nelson Mandela akiamka leo Kisha kumkuta Juan Mata akiwa katika benchi la Manchester United hana uhakika wa nafasi mbele ya Ashley Young, Valencia na Januzaj.
    Utahitaji kipawa cha khali ya juu kumuaminisha mtu aliyepofuka mwaka Jana kuwa Mata anazunguka mechi nne bila kuingia uwanjani lakini ndivyo ilivyo mchezaji ambaye alikuwa kipaji mpaka kufikia kuitwa Zola wa kispaniola yupo anaoza pale Old Trafford.

    Mchezaji aliyekuwa na uwezo wa kupiga pasi za mabao zenye wingi sawa na magoli ya Charlie Austin leo hana uhakika wa maisha ya soka.
    Mwandishi maarufu wa Marekani mwanamama Erma Bombeck aliwahi kusema katika moja ya nukuu zake kuwa Katika mwisho wa maisha yake atasimama mbele ya Mungu, na anaamini hatokuwa na chembe yoyote ya kipaji chake ambayo hakuitumia na angemwambia Baba nilitumia kila kitu ulichonipatia.
    Alikuwa sahihi sana,  umaarufu na heshima aliyojiwekea vingekueleza hiki,  hapa ndipo Mata alipo,  hili swali hata kwa Mungu litakuwa gumu Sana.
    Kwa kipaji cha Mata hajatumia walau nusu ya alichonacho. Bahati mbaya kwake sio yeye ambaye anaamua kutokutumia kipaji, bali ana waamuzi kabla yake.
    Tofauti na mwanamama Bombeck ambaye maamuzi yalikuwa ndani ya kalamu na mkono wake Mata maamuzi hayapo miguuni kwake, yapo akilini mwa makocha wake.
    Uwezo wa kukaba wa Valencia na young unaweka assist zake 15 kwa msimu benchi,  Uwezo wa Oscar na Willian kukimbia umbali mrefu uwanjani uliweka mchezaji bora Mara mbili mfululizo wa klabu benchi.
    Uliweka kipenzi cha mashabiki na wapenzi wa soka benchi. Mchezaji aliyewanyima Usingizi Carzola na Silva timu ya taifa akarudi benchi, akatulia.
    Bahati mbaya Sana kwa Mata, alikutana na wakufunzi viburi. Wasio sikia wala kuelewa. Dunia ya Leo usipopendwa na Mourinho au Van Gaal ama wasipokusajili wao unahitaji bahati ya Juu kuwa nacho wanachokitaka.
    Wao ni wale Wanaoamini kichwa Chao pekee. Mata hajawahi kuwa na nguvu ya Fellaini,  hawezi kukimbia mithili ya Hazard, na wala hawezi kaba kama Oscar lakini ana Uwezo wa kupika mabao ambayo ndo kazi yake ya awali maradufu kuliko wote hawa achilia mbali magoli anayoweza kukupa. Watu pekee ambao waliamini miguu yake hawakupendwa ama kukubaliwa na wamiliki.
    Di Matteo aliondoka, Benitez hakuongezwa mkataba na tuliyemtegemea kukirudisha kiwango chake David Moyes kibarua chake kilirithiwa mapema na Giggs kabla hajatulia akatua mbabe ambaye anaweza kumweka Rooney beki na wala usimwambie kitu.
    Ni dunia ya leo pekee ambayo Liverpool hawamuhitaji Mata kwa sababu ya Sterling au Markovic, na Manchester wanamlilia Fellaini dhidi ya Mata.
    Ni kama ambavyo Kwenye maisha ya kawaida tunavyohitaji gari la kutembelea kuliko nyumba ya kuishi.
    Mbabe wa zamani katika siasa na uongozi katika nchi ya Ujerumani Adolf Hitler aliwahi kusema Ufanye uongo uwe mkubwa, kisha Ufanye uwe mepesi, endelea kusema huo uongo Mara nyingi na mwisho wa siku watu watauamini. 
    Ni kwa staili hii ambayo alifanya watu waamini kuwa Ujerumani haikutakiwa kuchukuliwa kama nchi zingine kwa mfano wa mama au mwanamke bali mwanaume,.
    Uongo haswa lakini uliokuja kuaminiwa na kutumika, aliwaua waisraeli na kufanya ukatili ambao ulifanya kila nchi iamini Ujerumani in hatari achilia mbali ukatili wa Marekani pale Japan ambao haujawahi kujirudia.
    Hapa ndipo Mata alipo,  Mourinho alijaribu kusema, kisha akarudia, akafanya uwe rahisi na mwisho tukaamini amini kuwa mata hakuwa mkabaji kama Oscar, ni kama uongo wa Van Gaal ambao tumeuvumilia kisha kuukubali kuwa Young na Valencia wanakupa kitu cha ziada ambacho Mata hakupi au Fellaini kimo chake kinakupa mpango wa pili kufungua ulinzi wa upinzani.
    Bahati mbaya Sana Kuna uongo ambao unaweza Kuja kuaminiwa kuwa Mata anatakiwa kwenda Juventus kwa sababu kakosa nafasi.
    Mwisho atakosa jibu kwa Mungu kuhusu kipaji chake maridhawa kama mwanamama Bombeck, atasema nini wakati aliishia kufunga magoli 33 na kusaidia mengine 58 katika mechi 135 Chelsea wakati alitakiwa awe na zaidi ya hapo.
    Hata hivyo hakuna namna kama Hitler tu alivyosema, unadanganya, unasisitiza n unaufanya uongo uwe rahisi kisha unaaminiwa.
    Hata kwa Mata tumeamua kuamini,  tunafurahia magoli ya Erikssen pale Tottenham, Coutinho pale Liverpool na kusahau anayeyajua zaidi yupo benchi pale kwa mbabe Van Gaal.
    Ahsanteni.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Juan Mata: Tumesikia, Tumeona, na Tumeamini Uongo Uliosisitizwa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top