Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile
Media, Freddie Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji
kufikisha ujumbe muhimu kwa gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali
na kwa mtu binafsi.
Manento
alisema kuwa lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha
wafanyabiashara na sekta nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na
kujitangaza.
“Kama
ni mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa
muhimu utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo
ya biashara zao,” alisema Manento. “Ili kupata huduma hiyo, unatakiwa
kujiunga kupitia mtandao wetu, www.pushgw.com na kufungua akaunti yako,”
alisema Manento.
Alisema
kuwa makampuni au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa
wafanyakazi, wateja wao kuhusiana na biashara na taarifa nyingine. “Kwa
watu binafsi, unaweza kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli
mbalimbali ikiwa pamoja na harusi na hata kwa waandishi wa habari
wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la kuwasiliana na wahariri wao
kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,” alisema.
Mkuu
wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi
alisema kuwa huduma hiyo ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe
kwa kiasi cha sh 16 kwa kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.
Alisema
kuwa kwa upande wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na
madaktari kuwakumbusha wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu.
“Unachotakiwa kufanya ni kujiunga na huduma hii kwa njia ya mtandao na
kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa na
kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo
kuhusiana na huduma ya ‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma
hiyo itamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika
muda muafaka.
Mkuu
wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel
Mukundi (Kulia) akielezea umuhimu wa huduma ya “online bulk Messaging’
kwa sekta mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara
ya Ufundi.
Mkuu
wa Idara ya Ufundi wa Kampuni ya Push Mobile Media Daniel Buchafwe
akielezea jinsi ya huduma ya “online bulk messaging” inavyofanyakazi.
Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media
Limited, Ezekiel Mukundi.




